Taarifa mpya zinaibuka kutokana na shambulio la kutisha la mapanga huko Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwishoni mwa juma, ambapo watu kadhaa waliuawa akiwemo mtoto mchanga wa miaka miwili.BBC imefanikiwa kuzungumza na afisa mmoja ambaye alitaja shambulio hilo kuwa la "kushtua" katika eneo ambalo mara kwa mara hushuhudia viwango vya juu vya vurugu.
Furaha mwenye umri wa miaka miwili, Izaki mwenye umri wa miaka minne na Salama mwenye umri wa miaka minane walikuwa baadhi ya wahanga wa hivi punde katika mzozo unaoendelea.
BBC ilizungumza na Jules Tsuba, afisa wa eneo hilo katika eneo hilo ambaye aliripoti kuwa watu 14, wakiwemo watoto saba na watu wazima saba, waliuawa katika shambulio la Jumamosi dhidi ya kambi ya wakimbi.
Alililaumu kundi maarufu lenye silaha la Codeco, ambalo hapo awali limeshutumiwa kufanya mashambulizi katika eneo hilo, na alizungumza kuhusu athari mbaya ya mauaji hayo.
"Shambulio hilo ni la kushangaza," alisema. "Watu wetu wanapaswa kufa uzeeni, sio utotoni. Hatuwezi kustahimili hali hii.”
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇