LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 8, 2022

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMOS MAKALLA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA WAMAMA DUNIANI

Kwa hiki kidogo tumekuja kuwaletea nikwama tunawashukuru kwa kazi njema mnayoifanya, hii kazi mnayoifanya ni wito na niyaupendo kwa kuhudumia mtu aliyekosa matumaini na kumrudishi matumaini ni zaidi ya matumaini.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti TUGHE Taifa Dkt. Jane Madette mara alipoongozana na Wamama wa TUGHE wakiwa katika kuadhimisha Siku ya Wamama Duniani na kuwatembelea Wamama wenzao waliolazwa na watoto wao kitengo cha Saratani (Kansa) Hospitali ya Taifa Muhimbili na kukabidhi zawadi mbalimbali.

Hiyo niombe Wamama popote mlipo niwaombe sana kujitokeza Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla. 

Pia aliwatia moyo nakuwaombea kwa Mungu na bila kumsahau Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru kwa jinsi anavyojitoa nakujali kuwahudumia hawa wagonjwa na Asilimia kubwa wazazi wanatoka mbali na wengi niwenye kipato cha chini bila kujali Mungu ampe Umri mrefu pia na kumpongeza Kipenzi chetu Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi  Mkuu kwa kumuamini Mkurugenzi wetu.

Madette aliendelea kwa kusema'' lakini tunatambua tupo katika Siku ya Wamama Duniani amapo Kilele ni kesho Machi 8, 2022 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kwa sisi Wamama mnavyo tuona tumejipapasa kwenye mifuko yetu kwa namnatofauti nakupata hiki kidogo na tukapenda kuungana nanyi katika huduma mnayoitoa itasaidia kupunguza tatizo japo haitakwisha kabisa japo kwa Asilimia kidogo kwa hawa watoto.

Kwa kupokea hiki kidogo tunashukuru kama Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), pia tunawaomba mtuombee pia nasi tunawaombea mzidi kufanya kazi kwa weledi hawa watoke na kwenda kuungana na Familia zao napenda kusema asanteni sana na Mungu awabariki.


Afisa Muuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Asteria Henjewele alianza kwa kumshuru Mungu na kuwaomba Wamama hao kwa umoja wao wakiongozwa na Mwanamama mwenzetu Makamu Mwenyekiti TUGHE Taifa Dkt. Jane Madette kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), kwa hili tunawaomba mlibebe kutusaidia watu wakujitolea Damu kwa wagonjwa wetu wanauhitaji wa Damu na ninawasisitiza hili mlibebe na hata mwenye ndugu hata mmoja amlete natutamshukuru.

Pia napeda kutoa wito kwa Jamii matibabu ya mtu mwenye tatizo la Saratani  inatibika ukiwahi mapema na hasa ukiona dalili za mtu kutokwa na Damu mapuani,  homa za mara  kwa mara sio kumwambia mtuhuyo alale chali nikutokana na Jamii kutojua na unakuta mtu anafurahia kuona umewezesha kumuokoa mtoto.

Maombi ni muhimu kwenda ila msazi unashauriwa kuanzia Hospitali wakati huo mtu anaendelea na maombi mwingine anaenda kwenye maombi ajue anamchelewesha mtoto na wengine huanza kwa Waganga mtoto analetwa kesha chanjwa chale mwili mzima na inakua Saratani imeena mwiki mzima na inafikia mimi nalia kwanza watoto tunakaanao muda mrefu kwa kucheza nao. tunawazoea kwa hiyo wazazi ni mashahidi jinsi wanavyoumia nasi pia nizaidi kwenyenjia hiyo anayopitia mzazi sisi zaidi yao


Pia Kuna Tumaini la Maisha wanasaidia Dawa za Saratani (KANSA), kwa wanaofaham Dawa za Saratani Zinagharama ila Tumaini la Maisha wanatoa Dawa bila malipo yoyote hawaoi chochote hata ikija Bill ya Milioni Kumi inaandikwa barua kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tunataka nini yaani tumuache mtoto afe yani kiliochangu watoto waje kwa wakati aliendelea kusem''

Tunashukuru Muhimbili kwa kuendelea kutusaidia kwakutengeneza mazingira yanakuwa rahisi na yenye kufikika na pia mnavyokuja watu kamaniyi nakuchukua fulsa hii kuwaomba watu mbalimba, Makampuni mbalimba na watu mbalimbali kuwaletea watoto hawa chochote watakacho jaaliwa

Naomba mkimuona mtu huko mitaani mwenye dalili kama hizo na isije fikia hatua ya Tatu nawaomba tena kuwa Mabalozi na kuiambia Jamii Saratani inatibika kwa kuwahi Hospitali na pia matibabu ni bila malipo na tukisaidiwa na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru. mwisho nasema asanteni nikiwatakia Kwaresma njema na Mfungo mwema wa Mwezi wa Ramadhani unao tarajia hivi karibuni.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages