Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Dkt. Ritta Kabati amechangia tani 10 ya Saruji katika ujenzi wa nyumba za watendaji wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Iringa.
Kabati amekabidhi mifuko hiyo leo mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dkt. Edmund Mndolwa wakati alipokutana kuzungumza na watendaji mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Iringa katika ukumbi wa CCM Iringa mjini.
Aidha, Dkt. Kabati amesema ujenzi wa makazi mazuri kwa watendaji wa Chama utaleta tija katika ukuaji wa Chama kutokana na watendaji hao kuwa na mahali pazuri pakukaa na familia zao na hivyo kupunguza adha ya makazi wanayoweza kukumbana nayo.
Katika hatua nyingine Dkt. Kabati amewaomba viongozi wengine wakimo wabunge kujitoa katika kuhakikisha nyumba za watendaji wa Chama zinajengwa huku akiahidi kuendelea kuchangia zaidi hadi pindi zitakapomalizika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇