Na Eleuteri Mangi wa WUSM, Arusha
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango leo anafungua Kongamano la Pili la Matangazo ya Idhaa za Kiswahili Duniani, litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha ambapo aliwasili jana jijini hapa.
Kongamano hilo linawakutanisha Waandishi wa Habari na Watangazaji wa Idhaa zinazotumia lugha ya Kiswahili Duniani katika matangazo yake, kubadilishana uzoefu katika shughuli zao za kihabari ili kuleta tija zaidi katika kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha jamii.
Hadi sasa washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki kongamano hilo ambapo zipo Radio 45 za hapa nchini, 15 za nje, Televisheni 13 za kawaida na za mtandaoni, Televisheni 2 za nje ya nchi, Wahadhiri 20 wa Vyuo Vikuu vya ndani, wachapishaji watano, watu 16 mashuhiri kutoka ndani na nje ya nchi 16 na wanafunzi 200 kutoka vyuo vikuu vya jijini Arusha.
Washiriki wa Kongamano hilo wanatoka katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Malawi, Marekani, Rwanda, Ufaransa, Uganda, Ujerumani na wenyeji Tanzania.
Wazo la kuandaa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani lilianzishwa Novemba 29, 2006 na Kongamano la kwanza lilifanyika Novemba 12-15, 2007 lengo lake likiwa ni kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari ambavyo vinatekeleza jukumu la kukieneza Kiswahili duniani kwa kukitumia na kutangaza katika vituo vyao vya habari.
Your Ad Spot
Mar 14, 2022
Home
featured
Kitaifa
MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO KUFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA IDHAA ZA KISWAHILI DUNIANI, JIJINI ARUSHA LEO
MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO KUFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA IDHAA ZA KISWAHILI DUNIANI, JIJINI ARUSHA LEO
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇