LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 24, 2022

KIWANDA CHA VIFAA TIBA CHA MSAGARA INVESTMENT CHA BAGAMOYO, CHAPATA MITAMBO MIPYA YA KUZALISHA MARADUFU, CHAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA UWEKEZAJI NCHINI

Na Bashir Nkoromo, Bagamoyo
Kiwanda cha Vifaa Tiba cha Msagara Investment, kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani, kimenunua mitambo mipya 23 ya kisasa itakayokiongezea kiwanda hicho uwezo wa kutengenza kwa wingi zaidi  'Gauze' za mahitaji ya matibabu mbalimbali ikiwemo kufanyia upasuaji wa aina zote wa wgonjwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk. Ameir Binzoo amesema leo kwamba, wameamua kununua mitambo hiyo mipya ili kuongeza uzalishaji kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhimiza uwekezaji wa ndani na nje huku akiweka mazingira mazuri ya uwekezaji huo hapa nchini.

"Moja ya jambo ambalo limetusukuma kununua mitambo hii mipya, pamoja na kwamba tunawiwa kushughulikia afya za Binadamu wenzetu Watanzania na Nchi za Nje, lakini ni kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Rais wa awamu ya sita , Rais Samia na pia kutikia mwito wa Rais wetu wa kuhimiza wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza.

Hivyo tunamshukuru sana Rais Samia kwa kuweka mazingira mazuri ya Uwekezaji na pia Wizara ya Afya kupitia Taasisi zake zote  zinazohusika na masuala ya Afya na Vifaa Tiba  kwa ushirikiano waliotupa  katika kufanikisha upanuaji wa Kiwanda hiki.

Lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi  wa MSD  Brigedia Jenerali  Dk.  Gabriel  Mhidize  kwa MSD kuendelea kutupa ushirikiano na ushauri  wa jinsi ya kuboresha bidhaa zetu, kwa kweli huyu ni mzalendo wa kweli ambaye anapigania maslahi mapana ya  ya Taifa kwa kuonyesha nia ya kutaka kuona dawa na vifaa tiba vyote vinazaliwahshwa hapa nchini", amesema Dk. Binzoo.

Akizungumzia mitambo hiyo mipya Dk. Binzoo amesema sasa kiwanda kimefikisha uwekezaji wa mitambo yenye thamani ya jumla ya Sh Bililioni 4, na zina uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za 'Gauze' zenye ubora wa hali ya juu katika kufanya upasuaji wa aina mbali mbali na kufunga vidonda.

 

Amesema, thamani hiyo ya Sh. Bilioni 4 ya thamani ya mitambo iliyowekezwa ikiongezwa gharama ya Sh. Bilioni 3 zilizotumika katika upanuzi wa Kiwanda hicho Jumla ya uwekezaji uliofanyika ni Sh. Bilioni 7, na bado Kampuni hiyo inampango wa kuwekeza zaidi ikiwemo kuweka ghala Simiyu kwa ajili ya kununua malighafi ambayo ni pamba, moja kwa moja kutoka kwa wakulima.

Dk. Dk. Binzoo amesema Kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 2014 katika eneo la Mwananyamala kwa Kopa Jijini Dar es Salaam, kikiwa kidogo chenye uwezo wa kuzalisha 'gauze' tani 2,000 kwa mwezi, baada ya kupanuka na kujenga kikubwa zaidi katika eneo la Kilomo, Bagamoyo sasa kina uwezo wa kuzalisha gauze tani 20,000, kwa mwezi.

Amesema, pamoja na kuanza kutoa huduma za vifaa hivyo vya gauze kupitia MSD na Hospitali Binafsi, lakini hadi sasa kina uwezo wa kutosheleza bidhaa zake mahitaji ya hapa nchini na nje ya Nchi bila kutetereka.

"Uzalishaji wa kiasi cha tani 20,000 za 'Cotton gauze' kwa mwezi, ni kiwango kikubwa sana kwa mahitaji ya hapa nchini, hivyo tunaomba Serikali ituunge mkono kwa kutumia bidhaa zetu, kwa kuwa mbali na kukuza viwanda vya ndani na kukuza ajira lakini itasaidia Serikali kuondokana na matumizi ya fedha  za kigeni kwa kununua bidhaa hizi nje", amesema Dk. Binzoo.

Amesema, kufuatia kupatikana mitambo hiyo mipya Kiwanda hicho itazalisha tani 200,000 za gauze kwa mwezi zikiwa zenye ubora zaidi pengine kuliko hata bidhaa za nje, kwa kuwa zina uwezo kwa kutengeneza bidhaa kuanzia hatua za mwanzo kabisa na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu la mahitaji ya kisasa.

Dk. Binzoo amesema, tayari wameshaanza mazungumzo na Mamlaka za Nchi za Congo DRC, Rwanda, Burundi na Uganda kwa ajili ya kuuza katika nchi hizo bidhaa zao.

Mkurugenzi wa Masoko wa Msagara Investment Peter Ambilikile amesema, Wazo la kuanzisha Kiwanda hicho lilikuja mwaka 2012 baada ya Dk. Bizoo kupambana na changamoto ya Hospitali kukosa Gauze ya kufyonza damu baada ya upasuaji, alipokuwa anataka kumfanyia upasuaji mgonjwa katika hospitali moja jijini Dar es Salaam.

"Changamoto hii ilimtia simanzi na kumuumiza sana Dk. Binzoo, akawaza ni kwa nini bidhaa hizi za gauze ziwe adimu wakati malighafi yake ni pamba ambayo inalimwa kwa wingi hapa nchini, lakini inaishia kusafirishwa nje ya Nchi na baadaye kuletwa bidhaa zikiwa na gharama kubwa.

Baada ya kuguswa ndipo Dk. Bizoo Mwaka 2014 akaanzisha kiwanda hidogo katika eneo Mwananyamala kwa Kopa cha kuzalisha  Cotton Cauze kiasi kidogo tu cha tani 2,000 tu ambazo zilikuwa haziwezi kutosheleza soko la nje na hivyo Serikali ikawa inalazimika kuagiza nje", alisema Meneja Masoko huyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Vifaa Tiba cha Msagara Investment Kilichopo Kilomo, Bagamoyo mkoa wa Pwani, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea kiwanda hicho, leo. Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu Bahatisha Mashaka na Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda hicho Peter Ambilikile na kulia ni Mmoja wa Viongozi wa Kiwanda hicho Thabit Ameir.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo, akionyesha baadhi ya mitambo mipya iliyonunuliwa na Kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo akionyesha baadhi ya bidhaa za gauze zinazotengenezwa na Kiwanda hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Peter Ambilikile.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo akitazama mfanyakazi kwenye mashine ya kutengeneza gauze zenye kuambatanishwa mbili kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Peter Ambilikile.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo akionyesha  gauze zinazotengenezwa na kukatwa moja kwa moja vipande maalum.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Daktari Bingwa wa masuala ya upasuaji wa Binadamu Dk.  Ameir Binzoo (kushoto) akieleza moja ya mitambo ya kisasa inavyofanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda hicho.
Meneja Rasilimali Watu Bahatisha Mashaka (Kushoto), akieleza moja ya mashine za Kiwanda hicho zinavyofanya kazi kwa haraka na unadhifu mkubwa. (Picha zote na Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM)

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages