inayoonesha Jengo la Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba (bati za rangi za bluu na kijani) - hii Zahanati inapanuliwe iwe Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba.
WAKAZI na VIONGOZI wa Kisiwa cha Rukuba, Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru SERIKALI na RAIS , Mhe SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwapatia SHILINGI MILIONI 250 za ujenzi wa KITUO cha AFYA cha Kisiwani humo.
FEDHA hizi ni za TOZO ya miamala ys simu.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anafuatilia kwa karibu sana ujenzi unaoendelea Kisiwani humo na kwingineko Jimboni, na hadi kufikia leo (Jumamosi, 5.3.2022) maendeleo ya ujenzi Kisiwani Rukuba ni kama ifuatavyo:
*MAABARA - Msingi wa Jengo lake umekamilishwa leo. Picha 2 zimambatanishwa hapa.
*WODI YA MAMA & MTOTO - Msingi wa Jengo unajengwa na utakamilishwa wiki ijayo. Picha 1 imeambatanishwa hapa.
JENGO LILOJENGWA KWA NGUVU ZA WANARUKUBA & MBUNGE WA JIMBO
Hapo awali, Wakazi wa Kisiwani Rukuba (WanaRukuba) walianza ujenzi wa MIUNDOMBINU mipya ya kuboresha na kupanua Huduma za Afya zitolewazo na Zahanati ya Kisiwa hicho.
JENGO lilofikishwa kwenye renta litakamilishwa na matumizi yake yataelekezwa na Wataalamu wa Afya - Picha imeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇