Shilingi MILIONI 600 za UVIKO-19 zimetolewa, kupitia Mradi wa Bomba la Maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama, kwa ajili ya kusambaza maji kwenye Halmashauri 2 za Musoma DC (Musoma Vijijini) na Butiama. Fedha hizo zimegawanywa sawa sawa na kila Halmashauri kupata Shilingi MILIONI 300.
Kwa upande wa Halmashauri yetu, fedha hizo (Tsh 300m) zitatumika kusambaza maji ya bomba kutoka Mugango kwenda kwenye Vijiji vya Nyasaungu (Kata ya Ifulifu) na Kurwaki (Kata ya Mugango)
SHUKRANI nyingi mno zinatolewa kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan - wasikilize Wanakijiji wa Nyasaungu na Viongozi wao wakitoa shukrani zao.
Video/Clip imeambatanishwa hapa - tafadhali sikiliza.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇