LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 22, 2022

EU KUANZISHA JESHI LA PAMOJA LITAKALOTUMIWA WAKATI WA MIGOGORO

   Mawaziri wa mambo ya nje na wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya mpango wa usalama unaokusudia kuimarisha nguvu ya kijeshi ya umoja huo kwa kuanzisha jeshi la pamoja lenye hadi askari 5,000 litakalotumwa wakati wa mgogoro. 


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema katika taarifa kuwa, "vitisho vinaongezeka na gharama ya kutochukua hatua iko wazi," akisema mpango huo wa ulinzi unafaa kuwa tayari ifikapo mwaka 2030. 


Umoja huo umesema unahitaji kuwa na uwezo wa kulinda raia wake na kuchangia amani na usalama wa kimataifa kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Viongozi wa EU wanatarajiwa kutia saini mpango huo wa usalama, unaojulikana kama dira ya kimkakati, katika mkutano wa kilele utakaofanyika Alhamisi na Ijumaa mjini Brussels.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages