LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 23, 2022

CCM DODOMA YATOA MAAGIZO MAKUBWA UJENZI SOKO LA MACHINGA+video

 





Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Wazi la Wamachinga lililopo Barabara ya Bahi, jijini Dodoma Machi 22, 2022. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na Katibu wa CCM Mkoa, Pili Augustino.


Baada ya kumaliza kutembelea, viongozi hao walizungumza na vyombo vya habari ambapo walitoa ushauri na maagizo ikiwemo wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa muda uliopangwa  ambao ni Aprili 21, 2022.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Mkanwa aliliagiza jiji kuhakikisha  wanatafuta ufumbuzi wa haraka wa ni eneo gani watawajengea machinga takribani 600 watakaokosa nafasi katika jengo hilo ili isije ikasababisha tafrani. Jengo hilo litakuwa na uwezo wa wafanyabiashara 2900 wakati orodha kamili ya wamachinga walioorodheshwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni zaidi ya 3500.


Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, wakiangalia  mfano wa vibanda vitakavyotumiwa na wamachinga walipotembelea Soko la Wazi la Wamachinga Barabara ya Bahi, jijini Dodoma Machi 22, 2022.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Augustino akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukagua ujenzi huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akitoa ushauri na maagizo kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma  jinsi ya kuboresha ujenzi wa soko hilo.
Mchumi wa Jiji la Dodoma, Francis Kaunda akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Dodoma, Said Kasote  akitambulishwa.




Mafundi wakiendelea na ujenzi wa soko hilo ambalo kwa hivi sasa limefikia hatua ya kuezekwa.



 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri katika ziara hiyo na maagizo yaliyotolewa .......

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages