Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blog), imezidi kukomaa na hivyo kupata wadau au watu (Viewers) wengi wanaoiperuzi kila kisiku na kila muda ndani na Nje ya Tanzania.
Bila shaka Blog hii inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeweza kujipatia watu (Viewers) wengi wanaoisoma ndani na nje ya Tanzania kutokana na kuandika habari zake kwa umahiri na umakini mkubwa na kwa wakati.
Hivyo tunayo furaha kukujulisha wewe ambaye ni mdau mkubwa kuwa Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blog) leo Jumatano, Machi 9, 2022, imefikisha Watu (Viewers) Milioni 5, ambao huiperuzi kila siku na kila wakati.
Kwa kuwa nawe umekuwa miongoni mwa watu (Viewers) hao tunakushukuru sana, na tunakuomba uendelee kujipatia kwa wakati habari za ukweli na uhakika za CCM, Serikali na za Kijamii, kupitia CCM Blog.
Pia Mdau kumbuka habari zako za CCM, za Serikali zinazohusu Utekelezaji wa Ilani ya CCM, za Biashara na Uchumi na za Kijamii ukizituma kwetu na kuingizwa katika Blog hii zitasomwa au kuonwa na mamilioni ya watu (Viewers) hapa Tanzania na Nchi za Nje. Karibu.
Picha inayoonyesha Idadi ya Wasomaji (Viewers) hao. Kuona katika Blog yenyewe, Tafadhali, Bofya Hapo👉 CCM Blog
//Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu wa CCM Blog (0712498008)
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇