LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 6, 2022

RC MTAKA AWAZAWADIA WALIMU, WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI MATOKEO KIDATO CHA NNE+video

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewazawadia wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mkoani humo. Pia amewapatia zawadi za fedha walimu ambao masomo wanayofundisha wanafunzi wamepata alama ya A katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.


RC Mtaka akimpatia tuzo mmoja wa walimu ambao shule zao zilifanya vizuri matokeo ya kidato cha nne
RC Mtaka akielezea umuhimu wa elimu katika mkoa huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Maganga akielezea mpango mkakati wa kuboresha elimu mkoani humo.
RC Mtaka na Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe wakimpatia zawadi mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne 2021
Baadhi ya walimu, maafisa elimu na  wadau wa elimu wakiwa katika mkutano huo.
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Mwamfupe
Baadhi ya wanafunzi wa  shule ya sekondari Msalato wakiwa katika mkutano huo.
Ofisa Masoko wa  Benki ya NMB moja ya wadhamini wa hafla hiyo akielezea jinsi benki hiyo ilivyo mstari wa mbele  kuunga mkono juhudi ya kuboresha elimu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akielezea mpango wake wa kuwapeleka walimu na wanafunzi waliofanya vizuri  kwenda katika shule mbalimbali kufundisha mbinu walizotumia kupata ufaulu.
Mwenyekiti wa wakuu wa wilaya nchini, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Munkunda akielezea mpango mkakati wa kuboresha elimu wilayani kwake.
Mkuu wa wilaya ya Chamwino, Gift Msuya akielezea mpango mkakati wa kuboresha elimu wilayani kwake.
Mkuu wa wilaya ya Doidoma Mjini, Jabir Shekimweri akielezea mipango yake katika kuboresha elimu.


RC Mtaka na viongozi wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne 2021.

 RC Mtaka na viongozi wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule zilizofanya vizuri matokeo ya kidato cha nne.


PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, RC Mtaka akitoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa walimu na wanafunzi....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages