Mjumbe wa Kamati Tendaji Baraza la Vijana Zanzibar Amina Miraji amewasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Robo ya Kwanza ya Mwaka 2022 kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Mazingira na Watu wenye Mahitaji Maalum Jamila Borafia. Taarifa hiyo imewasilishwa leo tarehe 20 Februari 2022 mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Yunus Juma Ali
Tukio la uwasilishwaji wa Taarifa hizo za Kamati ulihudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano Mhe. Hamis Hamza Hamis
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais 9Muungano na Mazingira), Hamis Hamza Hamis.Faid Hamza Mjumbe wa Baraza la Watendaji Taifa
Asafu Sauph wakati wa uwaslishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Robo ya Kwanza ya Mwaka.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais 9Muungano na Mazingira), Hamis Hamza Hamis, akiwa na wajumbe wa waliohudhuria mkutano wa uwasilishwaji wa taarifa hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Baraza la Vijana Zanzibar limempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utendaji kazi wake huku likisisitiza kuwa kundi la vijana lina imani kubwa na wanamtakia heri na kumuunga mkono katika utendaji kazi wake.
Aidha, baraza hilo limempongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mariam Mwinyi kwa uzinduzi wa taasisi hiyo ambayo itaboresha maisha ya Wazanzibar.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa baraza hilo, Yunus Juma Ali wakati akipokea taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka 2022 ya utendaji wa kamati za baraza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita.
Katika taarifa za kamati, changamoto mbalimbali zimebainishwa kuwakabili vijana hasa wenye ulemavu ukwemo uchache wa watafsiri wa lugha ya alama, gharama kubwa za upatikanaji wa fimbo nyeupe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Mazingira na Mahitaji Maalum, Jamila Borafia amewasisitiza vijana kujiunga kwenye baraza hilo ili kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza, huku akiwaasa kujituma na kuondoa tamaa ya kifedha.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Yunus Juma Ali ametoa kauli hiyo jana tarehe 20 Februari wakati wa kupokea Taarifa ya Utekelezaji ya Robo ya Kwanza ya Mwaka 2022 kwa Kamati mbalimbali zilizomo ndani ya Baraza la Vijana Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇