LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 10, 2022

WAZIRI MKENDA, KATIBU MKUU SEDOYEKA WALAKIWA KWA SHANGWE WIZARA YA ELIMU+video

Waziri mpya wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (katikati) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Eliamani Sedoyeka (wa pili kulia) wamepata mapokezi makubwa walipowasili ofisi ya Wizara hiyo, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada kutoka kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino Januari 10, 2022.
Waziri Mkenda akikabidhiwa shada la maua mara baada ya kuwasili wizarani hapo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sedoyeka akifurahi kukabidhiwa shada la maua.
Naibu Waziri, Omary Kipanga akikabidhiwa shada la maua.
Waziri Mkenda akisalimiana na watumishi wa wizara hiyo wakati wa mapokezi.



Waziri Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Sedoyeka  wakilakiwa kwa furaha  na watumishi wa wizara hiyo.

Waziri Mkenda, Katibu Mkuu, Sedoyeka na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.




Waziri Mkenda akitia saini mara baada ya kuwasili ofisini kwake.
Katibu Mkuu, Sedoyeka akitia saini  mara baada ya kufika ofisini kwake
Waziri Mkenda akitia saini ofisini kwa Naibu Waziri Kipanga

 Katibu Mkuu, Sedoyeka akitia saini ofisini kwa Naibu Waziri, Kipanga


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.


Mdau, nakuomba uendelee kuona/ kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa mapokezi hayo......

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages