LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2022

WAZIRI BITEKO AIPONGEZA STAMICO KWA UFANISI, INASHINDANA TENDA ZA MADINI NA KAMPUNI KUBWA DUNIANI+video

Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) kwa kulifufua shirika hilo ambalo awali lilikuwa hoi bin taabani, lakini sasa limeongeza tija na hata kushindana tenda ya kuchoronga miamba ya madini na kampuni kubwa duniani. Ametoa pongezi hizo alipokuwa akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya shirika hilo katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dodoma Januari 15,2022. Asilimia kubwa ya bodi hiyo ina wajumbe kutoka bodi iliyopita ambayo imepambana kulifufua shirika hilo. Pia, utawasikia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Dkt. Venance Mwasse na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Meja Jenerali mstaafu Michael Isamuhyo wakieleza kupitia clip ya video hapo chini jinsi walivyopambana kulifufua shirika hilo.


Baadhi ya wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Stamico.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Meja Jenerali mstaafu Michael Isamuhyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Dkt. Venance Mwasse.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA 


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages