…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Zanzibar
Vigogo wa Soka nchini Simba na Yanga wanaanza leo kusaka taji la Michuano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea Visiwani Zanzibar katika uwanja wa Amaan.
Washindi wa pili wa Michuano hiyo timu ya Simba itashuka dimbani majira ya saa 10:00 kucheza na Selem View ambnao walianza kwa sare na Mlandege mechi yao ya kwanza huku wekundu wa Msimbazi itakuwa mechi yao ya kwanza wakiwa kundi C.
Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Timu ya Yanga watacheza na Taifa Jang’ombe majira ya saa 2:15 usiku,Taifa Jang’ombe walianza kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya KMKM mechi ya kwanza katika kundi B.
Matajiri wa Chamazi timu ya Azam FC wao walianza vyema jana usiku kwa kupata ushindi dhidi ya Meli 4 City bao peke likifungwa na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda.
Michuano hiyo ilizinduliwa mnamo Januari 3,2022 kwa mchezo mmoja wa Namungo dhidi ya Meli Nne City na Vijana wa kusini kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇