LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 16, 2022

SHAKA: RAIS SAMIA NI TURUFU YA MAENDELEO, ANATUMIA FALSAFA YA UPANGAJI, USIMAMIAJI NA UTEKELEZAJI

Na Mwandishi Maalum

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa turufu ya maendeleo ya Watanzania kutokana na falsafa iliyobeba mambo matatu anayoyatumia katika uongozi wake ambayo ni upangaji, usimamiaji na utekelezaji.

Shaka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akipokea tuzo ya kumpongeza Rais Samia kwa utendaji mzuri, iliyotolewa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alisema Rais Samia amekuwa turufu ya maendeleo ya watanzania kutokana na falsafa tatu anazozitumia katika uongozi wake ambazo ni upangaji, utekelezaji na usimamiaji.

Kwa mujibu wa Shaka, hayo yamejidhihirisha katika uongozi wake kwa kipindi cha miezi tisa ambapo mambo makubwa yamefanyika.

Alieleza katika kipindi hicho umeshuhudiwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025, kwamba wanaamini kufikia mwaka 2025 utekelezaji utazidi asilimia 100.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la UDSM, Isack Sambuli, alisema uamuzi wao huo unatokana na kuguswa na mambo makubwa anayoyafanya Rais Samia ambayo moja kwa moja yanawagusa wanafunzi wa elimu ya Juu na Watanzania kwa ujumla.

Alisema miongoni mwa mambo hayo makubwa ni pamoja na kuongeza fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu.

Sambuli alisema uamuzi wao huo haukulenga kutaka kutazamwa kwa ajili ya uteuzi wa uongozi Bali wamelenga kutazama uhalisia wa mambo makubwa.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM,Tawi la UVCCM Seneti Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam  Ndg Aizack Sambuli ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages