*Awatolea uvivu wanaoutaka Urais 2025, awaambia moyo wake sio wa glasi bali ni wa nyama
*Asisitiza hataacha kukopa kwa ajili ya maendeleo, ampiga kijembe Spika wa Bunge, agusia Serikali ya Mpito
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS Samia Suluhu Hassan amewaambia mawaziri,wakuu wa mikoa na viongozi Wengine wa ngazi mbalimbali kwamba anatarajia kutoa listi ya mawaziri na wakuu wa mikoa baada ya kuwasoma kwa kipindi cha miezi nane aliyokaa madarakani.
Amesema kuna baadhi ya mawaziri na wakuu wa mikoa ambao wanaoneka kuwemo kwenye harakati za kuutaka Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 huku akiweka wazi wenye nia hiyo atawaondoa wote ili wakajipange vizuri na mipango yao.
Ameongeza kuwa kuna mambo mengi yanayoendelea kutoka kwa viongozi ambao wenyewe wanaangalia mwaka 2025 na hivyo kuwa sehemu ya wanaokwamisha mipango ya maendeleo na baadhi yao ndio wamekuwa wakisema hakuna kinachofanyika lakini ukweli yeye ameapa kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo,hivyo haangalii mwaka 2025 bali kuleta maendeleo ya watu.
Akizungunza leo Januari 3,2022 katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa upokeaji wa ripoti ya matumizi ya fedha Sh.Trilioni 1.3 ambazo zimetolewa na Shirika la Fedha Duniani( IMF) ambazo ni mkopo usio na riba, Rais Samia ameshindwa kuweka kinyongo,hivyo ameeleza hatua kwa hatua kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa Serikali kuendelea kutumia vyanzo mbalimbali vikiwemo vyanzo vinavyotokana na fedha za tozo pamoja na fedha zinazotoka na mikopo kwa ajili ya kufanya maendeleo.
Hata hivyo amesema ameshangwaza kuona baadhi ya wanasiasa hasa wanaotokana na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakijenga hoja zq kuoneshwa kutofurahishwa na mikopo hiyo ambayo Rais amekopa na wala haina riba na ulipaji wake ni wa muda mrefu.
"Wapinzani wakisema wala hakuna tatizo, kwanza wapinzani wao wakitoa hoja zao na ukishazitekeleza wala hawana maneno, kazi iko kwa hawa wa kijani wenzangu, unashangaa kiongozi wa Muhimili wa Bunge akizungumza kuhusu mikopo,sawa ni maoni yake lakini lazima ufikirie,nilitegemea aunge mkono jitihada hizi.
"Lakini najua hayo yote ni kwasababu ya mwaka 2025, wanaangalia Uchaguzi Mkuu, mimi siangalii 2025 bali naangalia namna ya kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo, wao wanaoangalia 2025 waendelee tu,tutakutana huko huko.Wanazungumza kuhusu kukopa,sitaki kudanganya tutaendelea kukopa, hatutakuwa wa kwanza , tangu zamani tunakopa,kwanza maendeleo yetu ni ya kukopa kopa tu, tuna madeni lakini tunakopa na kulipa.
"Niseme tu sasa nina miezi nane madarakani ,nilikuwa nawasoma na ninyi mlikuwa mnanisoma, wakati nimefanya mabadiliko madogo katika Baraza la mawaziri nilisema nitawasoma mawaziri, leo nataka kuwaambia nitatoa list ya baraza la mawaziri na wakuu wa mikoa, wale ambao ninahisi wako pamoja na Mimi nitawateua na wale ambao hawako pamoja na mimi nitawaondoa ili mwende kujiandaa vizuri na 2025,"amesema Rais Samia.
Amesisitiza " Wale ambao wako pamoja nami katika kuleta maendeleo ya wananchi nitaenda nao na wale wenye kutaka uongozi 2025 nitawaacha.Kwanza uongozi hupangwa na Mungu na sio vinginevyo.Kwanza ndio hao hao ambao waliibuka mambo ya Serikali ya Mpita,tena walianzia huko huko Bungeni,lakini nikachukua Katiba nakuangalia hiyo Serikali ya Mpito nikasema mtakwenda na Samia."
Aidha Rais Samia amesema wakati viongozi wa ngazi mbalimbali wakizungumza amewasikia wakisema kwamba asivunjike,lakini ametumia nafasi hiyo kueleza wazi kwamba yeye moyo wake sio wa glasi, bali ni moyo uliotengenezwa kwa nyama, hivyo wala hawezi kuvunika moyo,aliapa kuwatumikia Watanzania ,hivyo ataendeleo na kazi hiyo.
Wakati anafafanua yayoendelea nchini Rais Samia amesema "Wamenitazama nilivyo wakajaribu, Mimi siko hivyo na wala sio wa kujaribiwa,lakini chakufurahisha wakati zinatolewa hoja kuhusu kukopa wako waliojibu na hao wamenipa moyo, hatuwezi kwenda na maendeleo ya ngazi za juu halafu tukaacha kushughulika na maendeleo ya wananchi wa chini,tutafanya maendeleo huku juu lakini na kule chini lazima tufanye.
"Wengine wanasema elimu imetupwa, hiki tunachofanya nini, tumepata fedha na tumeendelea kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya chini hadi elimu ya juu,wanaosema hivyo wamekosa la kufanya sasa wanafunua peji zile zile za zamani ,katika afya, maji ,umeme tutaendelea kuboresha , katika umeme sio hanasa ni lazima, watu waunganishiwe umeme kwa gharama zinazostahili."
Awali wakati Rais Samia anaanza kuzungumzia amesema baada ya fedha kugaiwa katika maeneo husika waliagiza fedha zitumike kwa malengo, kwani fedha hizo licha ya kuwa ni za kukopa lakini watanzania watazilipa huku akisisitiza ifikapo Januari 15 mwaka huu ujenzi wa madarasa nchini kote uwe umekamilika ili Januari 17 wanafunzi wote waende darasani.
"Nawashukuru sana najua kuna changamoto lakini mambo yamekwenda vizuri,hadi Desemba 31 ujenzi wa madarasa ulikuwa umefikia asilimia 50. Nawashukuru wote waliosimamia ujenzi, nawashukuru wote ambao wameutetea mkopo,Wengi wamejibu hoja, Gavana na timu take wamefafanua vizuri
"Dk.Mpango ametoa somo kidogo kuhusu mkopo , nawashukuru kwa uelewa wa pamoja, tunafanya maendeleo tukiwa na uelewa wa pamoja, nachotaka kusema fedha hizi zisimamiwe vizuri .Najua kuna maneno mengi yanasemwa huko, oooo fedha zinaliwa ,niliowakasimisha madaraka nendeni mkasimamie kuonesha fedha haziliwi kama baadhi ya watu wanavyosema".
Kuhusu tozo amesema kuwa zilipopitishwa kilele zilikuwa nyinyi lakini baada ya kupunguza tozo kelele zilipungua."Kuna wanaouliza kuna fedha ya tozo kwanini wanakwenda kukopa,lakini wahusika(mawaziri) wamejibu,nahitaji ya madarasa 10,000 kwa elimu ya msingi lakini yaliyojengwa kwa fedha za tozo ni madarasa 500 na hivyo lazima tukope kukamilisha majengo na hapo ni kwa elimu ya msingi tu bado hatuzungumzia elimu ya sekondari."
Ameongeza "Namshangaa watu wanaojua ukweli wanapotosha wanasema hoo kuna tozo lakini kwanini wanakopa, hatuwezi kujenga kwa fedha za tozo peke yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika hafla ya kupokea Taarifa ya Mpango wa awamu ya kwanza wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko 19 Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Januari 2022.
PICHA NA IKULU
Unatafuta kampuni halisi ya mkopo wa kifedha ili kupata mkopo wa euro 10,000 hadi euro 10,000,000 (kwa mikopo ya biashara au biashara, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya kibinafsi, mikopo ya nyumba, mikopo ya gari, mikopo ya uimarishaji wa madeni, mikopo ya mtaji wa mradi, mikopo ya afya nk. ))Au ananyimwa mkopo kutoka benki au taasisi ya fedha kwa sababu yoyote ile?Tuma ombi sasa na upate mkopo halisi wa kifedha. Imechakatwa na kuidhinishwa ndani ya siku 3. PACIFIC FINANCIAL LOAN FIRM
ReplyDeleteSisi ni wakopeshaji wa mkopo wa kimataifa ambao hutoa fedha halisi kwa watu binafsi na makampuni kwa riba ya chini ya 2% tukiwa na kitambulisho halali au pasipoti ya kimataifa ya nchi yako ili kuthibitishwa. Malipo ya mkopo huanza saa 1 (moja) baada ya mkopo kupokelewa. na muda wa kulipa ni miaka 3 hadi 35.
Kwa jibu la haraka na kushughulikia ombi lako la mpaka ndani ya siku 2 za kazi
Wasiliana nasi moja kwa moja kupitia barua hii: pacififinancialloanfirm@gmail.com
Wasiliana nasi kwa maelezo yafuatayo:
Jina kamili: ____________________________
Kiasi cha pesa kinachohitajika kama mkopo: _______________
Muda wa mkopo: ___________________________________
Madhumuni ya mkopo: ____________________
Siku ya kuzaliwa: ___________________________________
Jinsia: ______________________________
Hali ya Ndoa: ___________________________________
Anwani ya mawasiliano: ___________________________________
Mji / Msimbo wa Eneo: ___________________________________
Nchi: ______________________________
Kazi: ___________________________________
Simu ya rununu: __________________________
Tuma ombi lako la jibu la haraka kwa: pacififinancialloanfirm@gmail.com
asante
Afisa Mtendaji Mkuu :Pen Fed VICTORIA JOHNSON