LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 27, 2022

RAIS SAMIA AKATA KEKI KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA, IKULU JIJINI DODOMA, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikata keki kama kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo, Januari 27, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

 

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, ambapo amekata keki katika sherehe iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma.

Kwa kuwa ni siku muhimu kwa Rais Samia na kwa Watanzania ni vizuri tuitumie siku ya leo kumwelezea ili wengi wapate kumfahamu vema.

Rais Samia alizaliwa Januari 27, 1960 visiwani Zanzibar, sasa leo ametimiza miaka 62 na alipata elimu ya  msingi kati ya 1966 na 1972  katika shule tofauti tofati katika visiwa viwili vikubwa vinavyounda Kisiwa cha Zanzibar, ambavyo ni visiwa vya  Unguja na Pemba.

Samia Suluhu Hassani alianza safari yake ya elimu katika shule ya msingi  Chawaka  iliyopo kisiwani Unguja na  baadae alihamia shule ya msingi Ziwani  iliyopo kisiwani Pemba kabla ya kurejea kisiwani  Unguja na kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mahonda.

Elimu ya Upili ama Sekondari aliisoma kati ya mwaka  mwaka 1973 mpaka mwaka 1976 ambapo kama ilivyokuwa kwenye elimu ya msingi,Samia Suluhu Hassan alisoma shule mbili tofauti ambapo alisoma kidato cha kwa nza mpaka cha nne katika shule ya sekondari ya  Ngambo iliyopo visiwani Unguja  kati ya mwaka 1973-1975 kabla ya kuhamia sekondari ya na Lumumba, iliyopo kisiwani Unguja  mnamo mwaka 1976 ambapo alihitimu kidato cha nne.

Baada ya kumaliza elimu ya Sekondari,Samia Suluhu Hassan hakujinga moja kwa moja na masomo ya Chuo,kwani mwaka 1977, Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar ambapo alipanda mpaka  ngazi ya kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Wakati akiwa mtumishi katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,Samia Suluhu Hassan alikuwa akijiendeleza kielemu ambapo alisoma kozi fupi mbali mbali ikiwemo ya sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na Uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alihitimu stashahada ya juu ya Utawala mnamo mwaka 1986.

Kati ya mwaka 1992 mpaka 1994 Samia Suluhu Hassan alisoma stashahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Manchester kilichopo nchini Uingereza.

Kiu ya Samia Suluhu Hassan kujiendeleza kielemu haijawahi kufikia ukomo kwani mwaka 2015 alihitimu shahada ya uzamili katika maendeleo ya uchumi ya jamii katika program ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo kikuu cha Southern New Hampshire cha nchini Uingereza.

Samia Suluhu Hassan aliolewa miaka miwili tu baada ya kuhitimu elimu yake ya sekondari kule visiwani Zanzibar mnamo mwaka wa 1978, ambapo alifunga pingu ya maisha  Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo Wawili hao wamejaliwa watoto wanne ambapo Mmoja kati ya wanawe  Wanu Hafidh Ameir  aliyezaliwa mwaka 1982 ndiye anayefata nyayo za mama yake kwani , ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar

Samia Suluhu Hassan mbali na kuhudumu Serikalini tangu amalize masomo yake ya sekondari akiwa na miaka 16 alipata kufanya kazi na mshirika ya kimataifa ambapo kati ya Mwaka 1992 mpaka mwaka 1994 alifanya kazi na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa Chakula ambapo alihudumu kwa nafasi ya Afisa Miradi,Mbali na kufanya kazi Serikalini na katika shirika la umoja wa mataifa,Simia alipata kufanya kazi na taasisi zisizo za kiserikali kwa miaka karibu kumi akijikita zaidi katika harakati za usawa wa kijinsia

Alijiunga rasmi  na siasa mwaka wa 2000 wakati alipochakuliwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum, kuingia kwake kwenye siasa kuliifanya nyota yake kuanza kuchomoza katika medani za kisiasa na uongozi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya akateuliwa kuwa waziri wa  Afya, Jinsia na Watoto,uteuzi uliofanywa na Rais wa kipindi hicho Aman Karume.
Tansania President John Pombe Magufuli of Tanzania at State House in Dar es Salaam. Left is her vice president, Samia Suluhu Hassan.

Mwaka  2005 alichaguliwa tena kuwa mjumbe maalum na  kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya ya mapinduzi Zanzibar.

 

Mwaka wa 2010 alitia nia ya kuwania uwakilishi ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi huko Zanzibar.

Nyota ya Samia ilivuka mipaka kwani mwaka muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 alichomoza kwenye baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya  kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.

Machi mwaka 2014 Tanzania iliingia kwenye vuguvugu la kubadili Katiba yake ambapo huko nyota ya Samia ilichomoza tena, baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma.

 

 Samia alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%. Itakumbukwa Samia Suluhu Hassan wakati wa Bunge la Katiba kwani ndipo alipoanzwa kutabiriwa kushika nafasi ya juu zaidi ya kiutawala ambapo mmoja wa wajumbe aliwaasa wajumbe wamfikirie Mama Samia kwa nafasi ya juu zaidi kwenye uchaguzi uliokuwa unafuata wa mwaka 2015.

Nyota ya Samia Suluhu haikuwahui kuzimika wala kufifia kwani Julai mwaka 2015, Dk. John Magufuli  mara baada ya mpambano  mkali ndani ya CCM uliompa ushindi wa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchauzi Mkuu wa mwaka huo, mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu alimpendekeza Mama Samia kuwa mgombea mwenza wake na hatimaye baada ya uchaguzi Samia Suluhu Hassan aliweka historia nyingine ya kupanda katika siasa za Tanzania kwa CCM kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliomuweka katika historia nyingine ya kuwa Msaidizi Mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya Makamu wa Rais.

Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati akiomba ridhaa ndani ya Chama chake ili apeperushe tena bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huo, kwa mara nyingine alimpendekeza  Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wake ambapo ushindi wa chama chake uliilinda historia ya Mama Samia.

Sasa Rais Samia anakuwa  Rais wa Sita baada ya Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, ambapo ameshika nafasi hiyo ya juu kabisa ya kiutawala na kiuongoza baada ya kukidhi matakwa ya Katiba ya Tanzania.

 

 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages