Rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré azuiliwa katika kambi ya kijeshi
Hatua hiyo Inakuja huku kukiwa na mkanganyiko wa mahali alipo rais.
Shirika la habari la Reuters linavitaja vyanzo viwili vya usalama na mwanadiplomasia wa Afrika Magharibi wakisema kuwa alizuiliwa na wanajeshi waasi.
Milio ya risasi ilisikika hapo awali karibu na makao ya rais katika mji mkuu na milio ya risasi ikafyatuliwa katika kambi kadhaa huku kukiwa na uasi wa wanajeshi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇