Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa akizungumza na wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Ukombozi wakati wa ziara yake ya siku moja ya kujitambulisha na kujua changamoto zao tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya wilayani Iramba mkoani Singida jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida,Chone Malembo.
Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida,Chone Malembo (kushoto) ya upimaji wa dhahabu kabla ya kuuzwa katika Kituo cha Soko la kuuzia madini kilichopo Shelui wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Konkilangi wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa , akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mgodi wa Shinemine wakati akikagua mgodi huo wa uchimbaji wa dhahabu wilayani humo. |
Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini wa Mgodi wa Ukombozi Joseph Malyeta akizungumza kwenye ziara hiyo. |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Konkilangi, Mohammed Abbas akizungumza kwenye ziara hiyo. |
Muonekano wa Mgodi wa Shinemine kwa nyuma.
Naibu Waziri Kiruswa akioneshwa bwawa la maji yenye kemikali yanayotoka katika Mgodi wa Shinemine baada ya kutumika
Mkutano na Waziri ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mchimbaji Daud Lingo akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya Wachimbaji wa mgodi wa Ukombozi , Paul Ulaya akichangia jambo.
Mchimbaji Zahara Abdilahi akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mmoja wa Wakaguzi wa Mgodi wa Ukombozi, Amos Titus akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
NAIBU Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa ametoa muda wa siku 13 kwa Uongozi wa wilaya ya Iramba na Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kumaliza mgogoro uliopo kwenye kitalu namba 22 unaosababishwa na wanachama na wadhamini wa mgodi wa Ukombozi kutokana na mgongano wa kimaslahi.
Dk. Kiruswa ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi wa Ukombozi katika ziara yake ya siku moja ya kujitambulisha na kujionea baadhi ya miradi inayofanywa na wizara hiyo hasa katika sekta ya madini na kujuaaaaa changamoto za wachimbaji.
Dk.Kiruswa Baada ya kuzikiliza malalamiko ya pande zote mbili alisisitiza kuwa kama pande hizo hazitafikia makubaliano Serikali inaweza kufuta leseni hiyo na kutoa kwa mwekezaji mwingine ili uzalishaji uweze kuendelea.
" Natoa siku 13 kwa Uongozi wa wilaya ya Iramba na Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kumaliza mgogoro uliopo kwenye kitalu hicho katika machimbo ya Ukombozi vinginevyo Serkali inaweza kuifuta leseni hiyo" alisema Kiruswa.
Katika hatua nyingine Kiruswa aliupongeza Mkoa wa Singida hasa watendaji wa sekta ya madini kwa kuvuka malengo ya ukusanya wa maduhuli kwa mwaka huu wa fedha ambapo yalifikia asilimia 142.2 na kuwa hana mashaka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha mapato hayo yataongezeka kutokana na kufanya kazi vizuri.
Akijibu swali lililohusu wachimbaji wadogo kutopata leseni alisema kazi kubwa ya wizara kwanza ni kuwatambua,kujua idadi yao na wangapi wanaleseni kwani malengo la Serikali ni kusimamia sekta hiyo ya madini huku dhamira ni kuona kila mchimbaji anapata leseni na vifaa kama walivyoomba.
Pamoja na mambo mengine wachimbaji hao walimuomba Naibu waziri huyo kuwasaidia kupata umeme wa uhakika kutokana na uliopo kuwa na changamoto ya kukatika mara kwa mara.
Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida,Chone Malembo akizungumzia sifa za mtu anayepaswa kupatiwa leseni ya uchimbaji alisema sheria ya madini kifungu namba 8 kinaeleza anayeweza kupata leseni hiyo hata wachimbaji wadogo ili mradi awe ni mtanzania mwenye umri isiyopungua miaka 18.
Alitaja sifa nyingine kuwa ni awe hajawahi kushitakiwa au kutangazwa na mahakama kama amewahi kufilisika,awe na tini namba na kitambulisho chochot leseni ya udereva au cha uraia na awe na picha ndogo mbili aina ya pasipoti saizi.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda alisema katika mwaka wa fedha wa 2020/ 2021 waliweza kuzalisha gramu 319,000 na kuwa zimeweza kuiingizia fedha Serikali Sh.37 Bilioni ambapo mapato yaliyotokana na madini yalikuwa ni zaidi ya Sh.400 Bilioni.
Mwenda alitumia nafasi hiyo kuwaomba wachimbaji wa madini wilayani humo kuacha migogoro isiyo na tija badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kuongeza pato la Taifa kama walivyofanya katika kipindi cha mwaka 2020/2021.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇