Na Mwandishi Maalum
Mwanasheria Mkuu wa Mhe. Jaji Dkt Eliezer Feleshi jana (jumanne) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Wanasheria Wakuu na Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC).
Pamoja na mambo mengine katika Mkutano huo uliofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa njia ya mtandao, Wajumbe wa mkutano huo wamepitisha mabadiliko ya Ibara ya 9 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ( SADC Treaty) kwa kuongeza Bunge la SADC ili kuipa mamlaka Jukwaa la Bunge la SADC kuwa Bunge Kamili.
Vile vile Mkutano huo pia umepitisha Mkataba unaofanya mabadiliko katika Itifaki ya Utalii ( Draft Agreement amending SADC Protocoal on development of Tourim) na Kanuni za Dhamana ya usafirishaji wa mizigo katika Kanda ( Revised Regional Customs Transit Gurantee Regulations).
Katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu aliambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu , Ofisi ya Waziri Mkuu, Afisi ya Rais Zanzibar, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Nchi wanachama walioshiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao ni Angola, Botswana, Congo, Eswatini, Lesotho,Mozambique, Madagascar,Nambia, South Afrika, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.
Your Ad Spot
Jan 26, 2022
MWANASHERIA MKUU ASHIRIKI MKUTANO WA SADC KWA NJIA YA MTANDAO
Tags
featured#
Habari#
Share This
About Bashir Nkoromo
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇