LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 24, 2022

MABADILIKO YA TABIANCHI DUNIANI YAZUA MJADALA MKALI WAKATI WA MAFUNZO TGGA+video

 

Wakufunzi wakijadiliana jambo wakati wa mafunzo ya  mabadiliko ya Tabianchi yaliyoandaliwa na TGGA katika Baraza la Maaskofu (TEC), Kurasini jijini Dar es Salaam.

Wakufunzi wa Programu ya Mabadilikio ya Tabianchi Duniani wakilumbana kwa kila upande wa wanasayansi na wasioamini kuhusu mabadiliko ya Tabianchi kuvutia upande wake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao kuhusu namna ya kwenda kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kupambana na athari ya mabadiliko hayo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika katika Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), yamehudhuriwa na wakufunzi wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association,TGGA) kutoka mikoa 12 nchini na wengine kutoka Benin na Lesotho pamoja na wakufunzi wa kujitolea kutoka chama cha Girl Guides Duniani cha WAGGGS.

Meneja wa programu hiyo, David Mbumila mwishoni anaelezea jinsi walivyouandaa mjadala huo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo zaidi wa uelewa na namna ya kwenda kutoa elimu sahihi kwa jamii kuhusu mabadiliko hayo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages