Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo leo Jumanne Januari 11, 2022 amewasili Zanzibar kwa ajiri ya kushiriki sherehe za kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Afadhal Taib Afadhal
Sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar zitafanyika kesho tarehe 12 Januari, 2022 Katika uwanja wa Amani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇