Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, akiwa na VIONGOZI wa ujenzi wa Ifulifu Sekondari ya Kata ya Ifulifu katika kikao kilichofanyika Kijijini Kabegi, eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata.
Wanavijiji na viongozi wa Kata ya Ifulifu wanatoa shukrani nyingi sana kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuikumbuka Kata yao ambayo haina Sekondari yake kuwapatia sh. mil 470 za kusaidia kukamilisha ujenzi.
Ujenzi huo waliouanza mwaka 2017 unasuasua kwa ukosefu wa fedha.
Kata ya IFULIFU ya Jimbo la Musoma Vijijini yenye vijiji vitatu vya Kabegi, Kiemba na Nyasaungu ndiyo KATA PEKEE isiyokuwa na Sekondari yake, hali inapelekea wanafunzi kwenda kusoma sekondari za Kata jirani za Nyakatende na Mugango.
.Kijiji cha Nyasaungu kiko mbali na vijiji vingine na wakazi wake wengi ni wafugaji. Taarifa za ujenzi wa Sekondari ya Kijiji hiki cha Wafugaji ilitolewa jana, Ijumaa, 22.1.2022
UJENZI WA IFULIFU SEKONDARI
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba vilianza ujenzi wa Sekondari yao JUNI 2017
*MICHANGO ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:
(i) Wanavijiji - fedha taslimu na nguvukazi
(ii) Mbunge wa Jimbo - fedha zake binafsi
*MAJENGO yaliyokamilishwa kwa nguvu za WANAVIJIJI na MBUNGE wao:
(i) Vyumba viwili vya Madarasa
(ii) Msingi wa Jengo la Utawala umekamilika
(iii) Matofali 1,200 yametengenezwa
FEDHA ZA UVIKO- 19/IMF ZIMEPOKELEWA
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alienda Kijijini Kabegi kufuatilia ujenzi wa Ifulifu Sekondari na kujadili na Viongozi wa Kata hiyo kuhusu matumizi bora ya TSH MILIONI 470 walizozipokea kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
USHAURI ULITOLEWA NA MBUNGE WA JIMBO
*Vijiji 2 vya Kabegi na Kiemba vifanye VIKAO vya WANAVIJIJI kuwaeleza juu ya malengo ya fedha hizo (Tsh 470m) walizozipokea Katani
*Matumizi ya fedha hizo yawekwe wazi sana kwa wanavijiji
*Wanavijiji waendelee kuchangia nguvukazi ili miundombinu muhimu ya elimu ipatikane kutokana na fedha hizo.
*Ujenzi uende kwa kasi kubwa na kwa ubora unaokubalika
*Ifulifu Sekondari ifunguliwe Julai 2022., na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na kutoka Vijiji vya Kabegi na Kiemba waendelee na masomo yao kwenye Sekondari yao ya Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇