Kamati ya Ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Tumepokea vifaa vya ujenzi wa Ofisi yetu ambayo mda si mrefu itaanza kutumika.
Hadi sasa Jengo na Ofisi zote zilizopo humo ndani karibu asilimia 70% kukamilika.
Alhaji Salum Chima: Mhasibu
Kwa niaba ya Mkt wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi ya Chama Wilaya ya Ikungi naomba niwa pongeze washetiri wetu na kipekee Ninaomba kumshukuru Mhe. Elbarik Kingu Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi kwa utayari wake na majitoleo makubwa kwa kututafutia kiasi cha Shs 10 milioni Fedha hii imetuongezea nguvu kubwa katika kazi ya ujenzi ambapo tayari tumefanya kazi zifuatazo.
1. Tumejaza kifusi na Moram Ofisi zifuatazo Mkt, Katibu, Katibu mahususi na makatibu wote wa jumuia, store na jiko.
2. Tumepiga Lipu na sakafu Ofisi ya Mkt, Ktb na Katibu mahususi ndani na nje.
3. Tumefunga grili madirisha yote.
4. Tumefunga madirisha ya Aluminium ofisi za Mkt, Ktb na Secretary.
5. Tumeweka frem za milango 14 mahususi.
6. Tumefunga gpsum board ofisi za Mkt, Ktb na Secretary.
7. Tumefunga mifumo ya maji masafu na machafu ofisi ya Mkt na Ktb.
8. Tumejenga shimo la choo na mifumo yake ofisi ya Mkt.
9. Tumefunga miundombinu ya Umeme et condut pipe squerbox .
10. Tumefunga vyoo weastern type kwa Mkt na Ktb.
Pokea Shukrani zetu kwako.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇