Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface anasikitika kutangaza Kifo cha Mfanyakazi Mwenzake Bi. Suzan Kapinga (Principle Assistance Nursing Officer). Kilichotokea Januari 1, 2022 kutokana na Ajali ya Gari Maeneo ya Riverside.
Januari 3, Mwili wa Marehemu utaagwa kuanzia Saa 3.00 Asubuhi na Wafanyakazi wenzake, katika Taasisi ya Mifupa(MOI) na Baada ya kuaga Mwili Utasafirishwa Kuelekea Kimara Suka Alikokuwa Anaishi wakati wa Uhai Wake. Kutakuwa na Ibada ya Kumuombea Marehemu Nyumbani kwake Kimara Suka, ndugu, Jamaa na Marafiki Watatoa Heshima za Mwisho na Baadaye Safari Itaanza Kuelekea Mkoani Ruvuma, Wilaya ya Songea, Kijiji cha Namabengo, Ambako Ndiko Atahifadhiwa Katika Makaburi ya Kjiji cha Namabengo Siku ya Jumanne tarehe 4/1/2022.
Raha ya Milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie... Apumzike kwa Amani... Amina.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇