Muongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Florence Shimbi akielezea tabia ya Mbuni ndege mwenye mabawa lakini asiyeweza kupaa lakini ana uwezo wa kukimbia kwa kasi Km 70 kwa saa. Pia na sifa zake nyingine nyingi. Septemba 16,2021 nilibahatika kutembelea hifadhi hiyo nikiwa na viongozi wa Chama cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA) na kuzungumza na Mtalaam Florence ambaye alikuwa na mambo mengi ya kutuelezea kuhusu tabia za wanyama na ndege... . PICHA NA RICHARD MWAIKENDA MBUNI ni aina ya ndege,ila ndege huyu yuko tofauti sana na ndege wengine wote.Mbuni anatofautiana na ndege wengine kwa umbo pia hata tabia,Mbuni ni adui mkubwa wa binadamu na wanyama wengine wakali. Mbuni anayepatikana Afrika Mashariki ndiye ndege mrefu na mkubwa kuliko wote duniani,anakadiriwa kufikia urefu wa futi 9 na uzitowa kilo 156. Japo ndege huyu ana mabawa ila hana uwezo wa kuruka kama ndege wengine wenye sifa sawa ambao tumewazoea kuwaona wakiruka angani. 1: Uzito mkubwa wa Mbuni upo kwenye miguu yake ambayo ndio silaha yake kubwa dhidi ya maadui zake. Wataalam wanadai kwamba teke moja la Mbuni laweza kumuua binadamu na hata Simba. 2: Wakati hayawani na ndege wengine wakiwa na tumbo moja,Mbuni wana matumbo matatu. 3: Mbuni ndiye ndege mwenye kasi kuliko ndege wote hata wanyama wenye miguu miwili,kasi ya Mbuni ni km 70/saa na hatua moja ya Mbuni inaweza kufika hata mita 5. Mbuni ana kasi kuliko hata Farasi,Mnyama mwenye kasi zaidi kuliko viumbe vyote ni Duma, duma anauwezo wa kukimbia km 112 - 120/saa (70 - 75mph). 4: Yai la Mbuni ndilo kubwa kabisa kupita mayai ya ndege wote,likiwa na urefu wa sm 15.Yai hili pia ni gumu kiasi kwamba unaweza kusimama juu yake. Uzito wa Yai la ndege huyu ni takiribani kg 1.4 ambalo ni zaidi ya mara 20 ya uzifo wa yai la kuku na ili kupika yai la Mbuni hadi lichemke inachukua zaidi ya saa moja. Mayai ya Mbuni huatamiwa kwa muda wa siku 24 hadi kutotolewa vifaranga na kwa wastani Mbuni hutaga mayai kati ya 40 hadi 100 kwa mwaka. 5: Manyoya ya Mbuni yana historia ya kusisimua sana kwa sababu hapo zamani katika dola ya Misri ya kale yalikua yakitumika kama alama ya haki na kwa kipindi cha sasa yamekua yakitumiwa na wataalam wa mavazi kwa ajili ya kuweka nakshi kwenye mitindo mbalimbali ya mavazi. 6: Jicho la Mbuni lenye sm 5 ndilo jicho kubwa kuliko wanyama wote duniani,jicho hilo linamsaidia kuona mbali sana hasa maadui zake. Jicho la Mbuni ni kubwa kuliko hata ubongo wake. 7: Mbuni hawana meno,hivyo hutegemea sana mawe kusaga vyakula vyao.Mbuni hakosi kutembea na mawe popote,inasadikika kuwa Mbuni hutembea na mawe si chini ya kg 1. 8: Dume la Mbuni lina ngurumo kama za Simba. 9: Wanahistoria wengi wanaamini kuwa Mbuni wamekuwa wakiwindwa tangu maelfu ya miaka ya zamani,siyo kwa sababu ya nyama tu bali pia kwa uzuri wa manyoya yanayovutia sana. Tahadhari ni kwamba usicheze kabisa na Mbuni kwenye anga za mayai yake. 10: Mbuni ni ndege mwenye ushirikiano zaidi ya binadamu hasa katika kipindi cha kuatamia mayai,Mbuni hugawana majukumu ambako jike huatamia wakati wa mchana na dume wakati wa usiku. 11: Mguu wa Mbuni una vidole viwili vyenye kucha kwa mbele na kidole cha nje huwa hakina kucha (Ona katika picha ya tatu kulia),wakati ndege wengine huwa na vidole vitatu hadi vinne na uwepo wa vidole hivi humsaidia kuwa na mwendo kasi wa ajabu sana kuliko ndege wengine duniani. #Note:- Endapo ukitokea moto katika eneo alipotagia mayai yake,Mbuni anauwezo wa kuzima huo moto kwa kutumia maji.Huenda katika mto na kubeba maji katika mabawa yake kisha hurudi kwa kasi ya ajabu mpaka eneo la moto. |
Your Ad Spot
Jan 5, 2022
MFAHAMU MBUNI NDEGE WA AJABU HUKIMBIA KWA KASI YA KM 70 KWA SAA+video
Tags
featured#
makala#
Share This
About Author CCM Blog
makala
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇