Mkunga akiwa kazini.
Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania, limewataka Wauguzi na Wakunga kuzingatia ueledi, maadili na uwajibikaji muda wote wawapo kazini na kwamba atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni. Hayo na mengine mengi yamebainishwa na Msajili wa Baraza, Agnes Mtawa alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma Desemba 6, 2021, ambapo pia alielezea kuhusu mahafali ambapo wauguzi na wakunga 1224 wataapishwa na kupewa vyeti vya usajili na leseni katika sherehe itakayofanyika Jumatano Desemba 8, 2021 jijini Dodoma.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Msajili wa Baraza, Mtawa akielezea kazi za Baraza na Wauguzi na Wakunga wanvyotakiwa kuzingatia ueledi, maadili na uwajibikaji kazini na adhabu wanazoweza kupata endapo watakiuka mambo hayo.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇