LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2021

SHULE MPYA YA SEKA, MUSOMA VIJIJINI YAPATA TSH MIL. 80 YA UVIKO 19 KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA

SEKONDARI 22 za Kata 20 za Jimbo la Musoma Vijijini zimepewa Fedha za kujenga Vyumba vipya vya Madarasa. Ni kati ya Vyumba 4 (Tsh 80m) na 2 (Tsh 40m).


KATA ya 21 ya Jimbo letu ambayo haina Sekondari yake (Kata ya IFULIFU) na yenyewe imepewa fedha za kujenga Sekondari ya Kata yao - taarifa kamili baadae.


SEKA SECONDARI imefunguliwa Januari 2021. Sekondari hii ni ya PILI ya Kata ya NYAMRANDIRIRA yenye Vijiji 5 -  Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka.


Tafadhali sikiliza (CLIP iliyoko hapa) MAONI ya WANAVIJIJI na VIONGOZI wao kuhusu FEDHA za UVIKO 19 (IMF)


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages