Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Serikali imeahidi kuwatengea maeneo ya kuuza bidhaa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Wanawake Wajasiriamali Wadogo wa vikundi vilivyopo chini ya Kikundi cha Woman Of Hope Alive (WHA) kama njia ya kuwainua kiuchumi.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, katika Kongamano la 'Mwanamke na Vikoba' lililoandaliwa WHA, ambacho Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Dar es Salaam (CCM) Janeth Mahawanga, lililofanyika jana Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
"Ombi hili ni jema, nimelipokea, kwa hiyo katika Maonyesho yajayo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, tutawatengea nafasi maalum ya kuuza bidhaa zenu, hili halina shaka, kwanza ninavyowaona mlivyojizatiti naamini ninyi maonyesho haya yatawainua zaidi wengi wenu na kuwafanya kuwa wajasiriamali wakubwa", alisema Prof. Mkumbo na kuongeza;
"Jambo hili tulilifanya kwa Machinga, tuliwatengea eneo maalum la kuuza bidhaa zao katika Maonyesho yaliyopita ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, na walifanya vizuri, kwa hiyo hili halitashindikana kwenu, tutalifanya".
Prof. Mkumbo alitoa ahadi hiyo, akijibu maombi yaliyotolewa na Kikundi cha Women of Hope Alive (WHA), katika risala iliyosomwa na Katibu wa Kikundi hicho Sawera Mbwana, katika Kongamano hilo.
"Tunaiomba Serikali iweke utaratibu wa kuwasaidia kinamama Wajasiriamali Wadogo kuwa na maeneo ya kuuza bidhaa zao kila ufikapo msimu wa Maonyesho ya Biashara (Sabasaba), kwani wengi wao hutamani sana kupata nafasi hizo lakini kutokana na uwezo wa biashara zao kuwa mdogo wanashindwa kushiriki maonyesho hayo", alisema Katibu wa WHA katika risala hiyo.
Karika risala hiyo, pia WHA imeiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kuangalia namna gani inaweza kushawishi Viwanda vikubwa na Kampuni kubwa viwe na mtandao wa kibiashara uliounganishwa moja kwa moja na Wazalishaji Wadogo kwa lengo la kuwainua kiuchumi hasa kupitia Kikundi hicho cha WHA.
WHA iliomba pia Wajasriamali Wadogo nao kupitia kupitia EPZ wawezeshwe na Serikali kupatiwa elimu ya kukidhi matakwa ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi ikiwemo Mboga mboga zilizokaushwa na matunda pindi mradi mkubwa wa uwekezaji unaoendelea eneo la Kurasini, Temeke utakaojulikana kama Kurasini Industrial Park and Business Centre utakapokamilika.
Aidha katika Kongamano hilo ambalo vilishiriki vikundi 60 kutoka Kata zote 102 za mkoa wa Dar es Salaam, Prof. Mkumbo pia alizindua rasmi Benki ya Kikundi hicho cha WHA ya WHA Microfinance, ambayo Mwenyekiti wa WHA Mbunge Mahawanga alisema miongoni mwa faida za Benki hiyo itakuwa chachu ya kuwainua Wanawake wajasiriamali Wadogo kwa kuwapatia mikopo ya uhakika.
Katika Kongamano hilo ambalo ni la tatu kufanywa na WHA, mbali na mamia ya Wajasiriamali walihudhuria viongozi wengine mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Heri James, Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Msanja.
Kwenye Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa udhamini wa Ubalozi wa Uholanzi hapa Nchini, Kina Mama Wajasiriamali walinolewa na watoa mada kadhaa katika kuwajenga kifikra katika medani za Biashara na Uchumi, elimu ya namna ya kusajili Vikundi vyao.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, akizindua rasmi Benki ya Kikundi cha Women of Hope Alive (WHA) ya WHA Microfinance, katika Kongamano la 'Mwanamke na Vikoba' lililoandaliwa na Kikundi hicho na kufanyika Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa WHA Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Dar es Salaam (CCM) Janeth Mahawanga. na Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Msanja. Wanamuziki wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Bora Bora Sound wakitumbuiza, mwanzoni mwa Kongamano la 'Mwanamke na Vikoba' lililoandaliwa na Kikundi cha Women Of Hope Alive (WHA) kwa Udhamini wa Ubalozi wa Uholanzi na kufanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, jana.Nembo ya Women Of Hope Alive aliyokuwa ikionekana katika kona zote za Ukumbi wa Mlimani City, wakati wa Kongamano hilo.
Mratibu wa Kongamano la 'Mwanamke na Vikoba' lililoandaliwa na Kikundi cha Women Hope Alive (Chama Kubwa) Margareth Bonepastor akimkaribisha Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Janeth Mahawanga (kulia), kuzungumza na kufungua Kongamano hilo.Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam (CCM) Janeth Mahawanga, akizungumza na kufungua Kongamano hilo.
Washiriki wakiungana na Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga kusakata wimbo wa 'Wanawake na Mendeleo', uliopigwa na Bendi ya Bora Bora Sound, baada ya Mbunge huyo kufungua Kongamano hilo.
Baadhi ya Washiriki wakiwa ukumbini
Baadhi ya Washiriki wakijadiliana jambo mtandaoni wakati wa Kongamano hilo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kongamano hilo wakiwa ukumbini
Mtaalamu wa Mambo ya Kifedha kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi Janeth Hiza akionyesha Kitabu cha Mpango Mkuu wa Sekta ya Fedha, wakati akitoa mada kuhusu nidhamu ya fedha kwenye Kongamano hilo.
Meza ya Wasajili waliokuwa wakiingia kwenye Kongamano
Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hanya (Mama Makete), Naibu Katibu Mkuu wa UWT Mstaafu Eva Kihwele na Stella Walingozi kutoka UWT Wilaya ya Kinondoni.
Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam (CCM), Janeth Mahawanga akizungumzia mikakati ya Kikundi cha WHA kwa Waandishi wa habari, wakati wa Kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Msanja wakiongozwa na Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga walipowasili ukumbini.Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Janeth Mahawanga akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca MahundiKinamama wa WHA wakiwa wamejipanga kumlaki Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakati akiwasili kwenye Kongamano hilo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akiongoza na Mwenyekiti wa WHA. Mbunge Janeth Mahawanga alipowasili kwenye Kongamano hilo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Mkumbo na Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Kinamama wa WHA, baada ya kuwasili kwenye Kongamano hilo.
Prof. Mkumbo akiwasalimia Washiriki wa Kongamano wakati akiingia. Kushoto ni Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga.
Kinamama wa WHA wakifuatia kwa shangwe kumpamba Waziri Prof. Mkumbo baada ya kuwasili.
Waziri Prof. Mkumbo baada ya kuwasili meza kuu.
Afisa Biashara na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi Caroline Kibanga akizungumza wakati wa Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa udhamini wa Ubalozi huo.
Afisa Biashara na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi Caroline Kibanga na Afisa Kilimo na Biashara pia kutoka Ubalizi wa Uholanzi Thonestina Mutabingwa (kulia) wakimkabidhi zawadi ya Ubalozi huo, Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga kwa Jitihada zake za kupambana katika kuwainua Wanawake Kiuchumi.Afisa Biashara na Uchumi kutoka Ubalozi wa Uholanzi Caroline Kibanga akikabidhi risala yake kwa Waziri Prof. Mkumbo.Waziri Prof. Mkumbo akijadili jambo na Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga wakati wa Kongamano hilo.
Katibu wa Kikundi cha WHA Sawera Mbwana akisoma risala ya Kikundi hicho kwa Waziri Prof. Mbumbo.Kisha Katibu wa Kikundi hicho Sawera Mbwana akamkabidhi Waziri Prof. Mkumbo risala hiyo.Wageni Waalikwa na Washiriki wa Kongamano hilo wakiwa wameshimama kushangilia wakati katibu wa WHA Sawera Mbwana akikabidhi risala kwa Waziri Prof. Mkumbo,Waziri Prof. Mkumbo akizungumza kwenye Kongamano hilo kujibu risala ya WHA.
Mkurugenzi wa WHA, Mbunge Mahawanga akimsindikiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Heri James alipowasili ukumbini kwenye Kongamano hilo. Mkuu huyo wa Wilaya alichelewa kufika mapema kutokana na majukumu ya kikazi.
Waziri Prof. Mkumbo akisburi kufungua Benki ya WHA Microfinance. Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Heri James, Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Msanja (kushoto).Waziri Prof. Mkumbo akizindua rasmi Benki hiyo.
Waziri Prof. Mkumbo akiwa na Viongozi wa Kikundi cha WHA na Kina Mama wa Kikundi hicho kushangilia baada ya kuzindua Benki hiyo.
"Asante sana Mheshimiwa Waziri, WHA tumefarijika sana kwa kuja kutuunga mkono kwenye Kongamano hili", akasema Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga wakati akiagana na Waziri Prof. Mkumbo kabla ya kuondoka ukumbini.
Wakati Waziri Prof. Mkumbo akiondoka ukumbini shamra shamra zikatawala.Waziri Prof. Mkumbo akitazama Biadhaa zilizokuwa zikionyesha na Kinamama Wajasiriamali wadogo nje ya ukumbi baada ya kutoka ukumbini.
Waziri Prof. Mkumbo akitazama Biadhaa zilizokuwa zikionyesha na Kinamama Wajasiriamali wadogo nje ya ukumbi baada ya kutoka ukumbini. Wanne kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Heri James.Mkuu wa Wilaya ya Ilala Heri James na Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Mahawanga wakiwa na Kinamama wa WHA.
Mjasiriamali wa kutengeneza mapambo mbali mbali kwa kutumia vizibo vya soda, Modesta Ogunda, akimkabidhi zawadi ya upendo, Mnywekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga.
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇