LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 5, 2021

MWANTUMU MAHIZA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WENYE ULEMAVU DUNIANI MKOANI MOROGORO, AHIMIZA WAZAZI, JAMII KUWAJALI

Mlezi wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani yaliyofanyika Kimkoa wa Morogoro katika Uiwanja wa Shule ya Msingi Mwere, Manispaa ya Morogoro, jana Disemba 3, 2021. Mahiza amesema, "Walemavu wameiletea nchi sifa kubwa na wazazi watoeni watoto hawa majumbani, walimu msichoke kuwafundisha, hawa ni wenzetu, kuwepo kwao kunatuwezesha kuona ushiriki wao katika kuleta maendeleo katika jamii", amesema Mwantumu Mahiza.
Katibu wa Madiwani Manispaa ya Morogoro Salma Mbando ( aliyevaa gauni la kijani) pamoja na Diwani wa Kata ya Mkundi, Seif Chomoka ( aliyevaa suti) wakimuongoza Mlezi wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza kuingia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika Kimkoa wa Morogoro katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwere, Manispaa ya Morogoro Uwanja, Disemba 3, 2021.
Wananchi wakiwa wenye Maadhimisho hayo.
Wananchi wakiwa wenye Maadhimisho hayo.
Vijana wa Skauti wakiwa na bango la Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani yaliyofanyika Kimkoa wa Morogoro katika Uiwanja wa Shule ya Msingi Mwere, Manispaa ya Morogoro, jana Disemba 3, 2021.
Katibu wa Madiwani Manispaa ya Morogoro Salma Mbando (Wapili kulia, mstari wa mbele) na Diwani wa Kata ya Mkundi, Seif Chomoka ( aliyevaa suti ya bluu) wakiwa na Mlezi wa Skauti Tanzania, Mwantumu Mahiza katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kimkoa wa Morogoro ilifanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwere, Manispaa ya Morogoro jana Disemba 3, 2021.
Maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Wenye Ulemavu Duniani,  ambayo Kimkoa wa Morogoro yalifanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwere, Manispaa ya Morogoro jana Disemba 3, 2021.


 Sikiliza Ujumbe wa Mwantumu Mahiza Hapo👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages