Na Bashir Nkoromo. Temeke
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave amewahimiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali wa ngazi zote kudai ushirikishwaji katika hatua mbalimbali maeneo yao jimboni humo yanapokuwa yanapatiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji miradi.
Amesema hatua hiyo ya kudai ushirikishwaji itawawezesha viongozi hao kujua kiasi cha fedha zinazopatikana ili kulinganisha kama kweli zinakuwa zimetumika kutekeleza miradi kulingana na thamani halisi ya fedha husika badala ya kuachiwa watu wachache ndiyo wafahamu kiasi cha fedha na miradi.
Mbunge Kilave ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipokuwa katika ziara kufuatilia na kukagua miradi iliyotekelezwa au kuendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali katika Kata ya Mtoni katika Jimbo hilo la Temeke, leo.
Katika ziara hiyo ambayo ni mwendelezo wa ziara za aina hiyo alizozianza mwezi uliopita, Mbunge Kilave alifuatana na Kamati ya Siasa ya CCM, Sekretarieti, Mtendaji wa Kata ya, na Wenyeviti wa Mitaa Kata ya Mtoni Mbunge Kilave alikagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vinavyojengwa kwa thamani ya sh. milioni 40 katika Shule ya Sekondari Relini.
Mbali ya shule hiyo pia Mbunge Kilave alikagua Soko la Kisasa ambalo linajengwa katika Kata hiyo kwa fedha zilizotolewa na Serikali kupitia maombi ya mbunge huyo ambapo katika mazungumzo ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa soko hilo na vyumba hivyo vya madarasa,
"Kwanza kabisa tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutujali wana jimbo hili la Temeke, sasa fedha hizi ni nyingi, kwa hiyo lazima vyumba hivi vijengwe kisasa kabisa, na sakafu yake isiwe ya saruji tu, hakikisheni inakuwa sakafu ya malumalu", akasisitiza Mbunge Kilave na kuongeza;
" Mnajua ninyi viongozi wenzangu hasa wa Chama Cha Mapinduzi ni lazima kuwa mnadai kushirikishwa katika hatua zote pale fedha zinapoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, siyo kujiweka pembeni halafu mambo hakienda hovyo ndiyo mnaaza kulalamika, siyo haisaidii".
Mwanzoni mwa ziara hiyo Mbunge Kilave alikutana na kuzungumza na viongozi wa CCM kata ya Mtoni katika Ofisi ya CCM ya Kata hiyo, na baadaye alifanya kikao kingine katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mtoni ambapo walishiriki pia Watendaji wa ngazi mbalimbali akiwemo Mtendaji wa Mtaa na viongozi wa Ulinzi na Usalama katika kata hiyo.
Katika vikao hivyo walijadili mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo baadhi yake zilipztiwa majibu na wahusika na nyingine aliahidi kuzifanyika kazi ili kuhakikisha jimbo la Temeke linakuwa lenye maendeleo na kukalikakwa amani na utulivu.
Simulizi katika kuhusu ziara hiyo👇
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akissisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi wa CCM mwanzoni mwa ziara yake katika Ofisi ya CCM Kata ya Mtoni jimboni humo kuanza ziara hiyo.Mmoja wa viongozi Kata ya Mtoni akimwambia Mbumbe Kilave baadhi ya changamoto zilizopo katika Kata hiyo
Kisha Mbunge Kilave na msafara wake wakatinga Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mtoni.
Akasaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Kata kata hiyo ya Mtoni Anaclet Hayuka.
Afisa Mtendaji Kata ya Mtoni Anaclet Mayuka akimsomea Mbunge Kilave (Wapili kulia), taarifa ya hali ya Kata hiyo
Mbunge wa Jimbo la Temeke Mama Kilave akapata nafasi ya kuzungumza na watendaji wa Serikali na Wa CCM katika Kata hiyo.
Mkuu wa Polisi Kata ya Mtoni S/SGT Bedas Mulimuka akizungumzia hali ya Usalama na Amani na changamoto mbali mbali za kiulinzi na usalama katika Kata hiyo mbele ya Mbunge Kilave.
Wasaidiwzi wa Mbunge Kilave katika kikao hicho
mMmoja wa viongozi katika Mtaa ndani ya kata hiyo ya Mtoto akizungumzia changamoto cha ulinzi na usalama wakati wa kikao hicho cha Mbunge Kilave.
Baada ya Kikao hicho Mbunge Kilave akatinga shule ya Sekondari Relini👇
Mbunge Kilave akitoka kukagua vyumba hivyo vya madarasa
Muonekano wa nje wa vyumba hivyo vya madarasa.Mbunge Kilave kisaini juu ka juu kitabu cha wageni baada ya kukagua ujenzi wa vyumba hiyo.
Mbunge Kilave na msafara wake wakitoka kwenye Shule hiyo baada ya kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa. Kisha akaingia mtaani na kusikiliza papo hapo changamoto zinazowakabili na wananchi.👇
Akafika kwa mjasiria mali wa ufundi wa kushona nguo, akazungumza naye mawili matatu, inagawa yeye hakueleza changamoto zinazomkabili katika shughuli zake.
Kisha Mbunge Kilave akatua kwa Mwanadada mpamgaji, katika mtaa wa Kweli, " Vipi na mimi nionje chips zako kidogo?" Mbunge Kilavu akamuuliza mwanadada huyo, naye akamwambia " Chukua tu Mheshimiwa Mbunge wetu hapa ni kwako".
Mbunge Kilave akaonja kidogo, Mwanadada akafurahi na kushangilia.
"Ohh tamu mno", akasema Mbunge Kilave, huku mwanadada huyo akiendelea kufurahia tukio hilo.
"Mama ukitaka shughuli zako zikue chukua mkopo wa Halmashauri, hauna riba, nenda kwenye vikao vinavyozungumzia mikopo katika Kata yako, usizubae ni fursa ambayo ipo wazi", Mbunge Kilave akamwambia Mamalishe mwingine katika mtaa huo wa Sawa.
"Haya na wewe Bodaboda unasemaje?" Mbunge Kilave akamhoji dereva wa bodaboda katika mtaa huo wa Sawa. akajibu "hamna shida Mheshimiwa tupo vizuri".
"Haani huyu Mheshimiwa Kilave yupo vizuri mno, ni mchapakazi na tena ni mtu wa watu". bodaboda huyo akasema kumwambia mwenzake
Mbunge Kilave ikabidi aangushe tabasamu kwa boda boda huyo.
"Binti hujambo?" Mbunge Kilave akimsalimia mwanadada fundi wa kushona nguo katika mtaa huo wa Sawa."Mheshimiwa mtaani kwetu hapa kuna kero ya maji kutiririshwa hovyo tunaomba utusaidie", akasema mwana mama huyu naye mbunge akajibu "Nimelipokea hilo nitalifanyia kazi na wenzangu".
"Na wewe shughuli zako zikoje", Mbunge Kilave akamuuliza huyu mama mkanga mihogo na vyakula vingine vidogo vidogo katika mtaa huo wa Sawa. akajibu "Zinaenda vizuri tu, ila tunaomba tusaidie kupata mikopo".
" Sawa mikopo inapatikana, unachotakiwa kufanya fuatilia kwa viongozi wa mtaa awako na Kata, ili upate maelezo ya kina, na pia kwenye vikao usikose kuwa unahudhuria maana huko ndiyo unaweza kujua mengi", Mbunge kilave akamuelimisha mama huyo
KISHA AKAKAGUA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA KATA HIYO YA MTONI👇 |
nn
nnn
n
n
n
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇