LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 11, 2021

MBUNGE KILAVE ALIPOKUTANA NA 'SAPRAIZI' YA 'HAPPY BIRTH DAY' YAKE, AKIWA KATIKA ZIARA YA MWISHO KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI TEMEKE, JUZI.

Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dorothy Kilave akikata keki ya 'Happy Birth Day' yake, baada ya keki hiyo kuletwa na wajumbe ukumbini ghafla, mwishoni mwa Kikao chake na Kamati ya Siasa ya CCM Kata ya Miburani, ambako alifika ikiwa ni ziara yake ya mwisho ya kufuatilia na kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali pamoja na Mfuko wa Jimbo lake, juzi, Disemba 8, 202. Ziara hiyo aliianza Novemba 22, 2021 kwa kutembelea kata zote jimboni.

Kabla ya Keki hiyo👇

Mbunge Kilave akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Kata ya Miburani. Kulia ni Katibu wa CCM wa Kata hiyo Amir Matimbwa na Kushoto ni Diwani Kata ya Miburani Juma Mkenga na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Ally Mkoyogole.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Kata hiyo wakiwa ukumbini wakati wa Kikao hicho. Mara keki ikawekwa mbele ya Mbunge Kilave👇
"He jamani, mbona mmeninistukiza, hata sikujua kama mnajua leo ndiyo 'Birth Day' yangu", Mbunge Kilave akasema huku akionyesha mshangao kidogo na kuongeza; Asanteni kwa upendo mlionionyesha".
Diwani wa Viti Maalum (CCM) Nuru Cassian akafungua Shampeni fasta, huku akishangiliwa kwa kinywaji hicho kufunguka vizuri huku kikilipika, Paaa!
Diwani Nuru Cassian akakisogeza kinywaji hicho kwa Mbunge Kilave, lakini iikabidi kinywewe na wengine kwa kuwa yeye alikuwa amefunga swaumu maalum.
Akaikata keki..
Akatenga vizuri vipande kwa ajili ya kuwalisha wajumbe mbalimbali,
Shangwe ikatawala ukumbini.
Nyuso za furaha zikaonekana wakati Mbunge Kilave akiandaa vipande vya Keki ili kuwalisha.
"Haya Mwenyekiti naanza na Wewe", Mbunge Kilave akasema wakati akimlisha kipande cha Keki Mwenyekiti wa CCM Kata ya Miburani Ally Mkoyogole.
Halafu akalishwa Diwani wa Miburani Juma Mkenga.
Kisha Katibu wa CCM wa Kata hiyo ya Miburani Amir Matimbwa.
Mbunge Kilave akaendelea kulisha keki hadi ikafika zamu ya Diwani wa Viti Maalum (CCM) Kata ya Miburani Nuru Cassian.
Halafu akalishwa Diwani mwingine wa Viti Maalum Scolastica Chuma.
"Haya Kaka yangu, na wewe pata hii", akasema Mbunge Kilave akimlisha keki kijana huyu.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mibulani Adili Awadhi na yeye hakubaki nyuma, akalishwa keki.
Keki yenyewe ilikuwa ya kiwango cha TBS, ndo hii.
Baada ya shamra shamra hiyo, Mbunge Kilave alitoka ukumbini akiambana na Diwani wa Viti Maalum Nuru Cassian.

Mbunge wa Temeke Mama Kilave akisaini kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Miburani Macelina Kimario (kulia).
Mbunge Kilave akazungumza na baadhi ya Walimu mambo ya msingi.

Mbunge Kilave akapiga na Walimu  hao picha ya kumbukumbu
"Mheshimiwa ukatusemee huko, tazama moja ya viti tunavyotumia hapa ofisini", akasema Mwalimu mmoja.
Kisha Mbunge Kilave akawaaga
Akaanza kukatiza chocholo kwenda kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwenye shule hiyo kwa fedha za Uviko 19.

"Enhee, hili dirisha limekaa vizuri, tena linaonekana litakuwa imara", akasema Mbunge Kilave wakati akikagua madirusha hanayotumika kujenga vyumba hivyo vya madarasa.
"Kwa hiyo madarasa haya hatawekwa 'tiles' ili yadumu au siyo", akauliza Mbunge Kilave na kujibiwa na Mwalimu Kimario (kulia), "Ndiyo". Kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Nuru Cassian.
Mbunge Kilave akaamua kusaidia kidogo kupiga ripu katika ujenzi huo.
Kisha akasaidia pia kuchanganya mchanga na saruji.

Diwani Kata ya Miburani Juma Mkenga naye akamuunga mkono Mbunge Kilave.
Diwani Nuru Cassian naye hakukubali kupitwa , akamuunga mkono Mbunge Kilave.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Miburani Adil Awadh naye akamuunga mkono Mbunge Kilave.
"Haya sasa tunaenda Shule ya Sekondari Kibasila, au siyo?", Mbunge Kilave akamwambia Afisa Mtendaji Kata hiyo ya Miburani Msiya Ngowi (aliyebeba mkoba).
Mbunge Kilave akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Stephen Mtulo, kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa hela za Uviko 19.
"Haya twende tukakague", akasema Mbunge Kilave kuuambia msafara wake.
Mbunge Kilave akiingia kwenye moja ya darasa linalojengwa.
Mbunge Kilave akizungumza na fundi ujenzi na kutazama ujenzi unavyoendelea katika moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa  kwenye shule hiyo ya Kibasila.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Stephen Mtulo, akieleza kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa hela za Uviko 19.
Mbunge Kilave akiondoka katika shule hiyo ya Kibasila baada ya ukaguzi.
Mbunge Kilave na Diwani Nuru wakipiga shoto kulia kuendelea na ziara.
Diwani wa Kata ya Miburani Juma Mkenga akimaptia maelezo Mbunge Kilave kuhusu maendelea ya Zahanati
Afisa Mtendaji Kata hiyo ya Miburani Msiya Ngowi (kulia) akimpatia maelezo Mbunge Kilave kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Miburani

"Haya jamani nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa, hapa ndiyo nimehitimisha ziara yangu, Lakini hapa Miburani ni nyumbani, nikipata nafasi nitakuwa napita pita kuona maendeleo na kuwasalimia", akasema Mbunge Kilave mwishoni mwa ziara yake. Halafu zikafuatia Picha za kumbukumbu👇
👇
👇
👇
👇
Mbunge Kilave akiwa katika picha ya kumbukumbu na Kamati ya Siasa Kata ya Miburani, mwishoni mwa ziara yake.
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages