Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo Wilayani Ubungo katika mkoa huo, Uliofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo Cha Usafirishaji (NIT), Mabibo, leo.
Mwenyekiti huyo wa CCM ameupongeza Uongozi wa UVCCM Kata hiyo kwa namna walivyokuwa wabunifu katika maandalizi na kuufanikisha Mkutano huo kwa hadhi ya hali ya juu, kwa kuweza kukutanisha Wajumbe wengi na Waalikwa wengi pia.
Kufuatia kuridhishwa kwake na Mkutano huo, Mama Kamba amewataka Viongozi wengine wa Jumuiya hiyo kuiga mfano wa UVCCM Kata ya Mabibo, pia pamoja na mambo mengine ameahidi kuwatafutia mradi ambao watauendesha Vijana hao wa UVCCM Mabibo kupitia mchakato atakaowaelekeza.
Akizungumzia Suala la Mikopo ambalo amekuwa akilifanya Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Rais yupo sahihi hivyo Vijana na Watanania wote wamuunge mkono Rais ili asivunjwe moyo.
Mapema Katibu wa UVCCM Kata hiyo ya Mabibo Abulauf Mkonga alisema katika Risala kwamba Mkutano umeambatana na kufanyika asubuhi ukaguzi wa miradi ya maendeleo kupitia kampeni ya Mkutano huo ya 'Duka la Mama lina bidhaa nzuri',
Akifafanua maana ya kaulimbiu hiyo alisema Didhaa hio ni Miradi ya Maendeleo na kwamba Wauzaji wakuu wa bidhaa hiyo kwenye duka ni viongozi ni Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Diwani Kata ya Mabibo na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
Katibu huyo wa UVCCM alisema miongoni mwa bidhaa hizo ni miradi iliyofanyika katika Kata ya Mabibo ambayo mi pamoja na Barabara ya lami kutoka Chuo cha NIT-Mburahati-Magomeni, Matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Mabibo.
Mingine aliitaja kuwa ni Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Mabibo, Ukarabati wa Barabara ya lami Mabibo-Big Brother, Madarasa manane katika Shule ya Sekondari Mabibo na Uzio katika Shule ya Msingi Mpakani.
Picha zaidi za Mkutano huo👇
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akisindikizwa na Viongozi wa UVCCM Kata ya Mabibo kwenda ukumbini baada ya kumpokea.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akiingia ukumbini.Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Kata ya Mabibo akihamasisha shangwe wakati Mama Kate Kamba akiingia ukumbini.Mgeni rasmi Mama Kate Kamba akiwa tayari meza kuu kwenye mkutano huo. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Ndugu Mgonja na kushoto ni Katibu wa UVCCM Kata ya Mabibo Rauf Mkonga na Mwenyekiti wa UVCCM Kata hiyo Nassibu Mangushi.
Wajumbe wakishangilia kumlaki mgeni rasmi
Wajumbe wakishangilia kumlaki mgeni rasmi
Wajumbe wakiwa wameketi baada ya mgeni rasmi kuketi
Wajumbe wakiwa wameketi baada ya mgeni rasmi kuketi
Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Kata ya Mabibo Abdullatif Maundu akifanya utambulisho.Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Mama Kate Kamba akimuuliza jambo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mabibo Nassibu Mangushi.
Katibu wa UVCCM Kata ya Mabibo Raufu Mkonga akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mwenezi Hilda Martin akifanya utambulisho
Diwani wa Kata ya Mabibo Joseph Klerruu akisalimia baada ya kutambulishwa. Diwani huyo pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya CCM ya Jitegemee.
Katibu wa CCM Kata ya Mabibo Juma Shabani akizungumza katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya ya Ubungo Yussuf Ramadhani akizungumza katika mkutano huo
Katibu Mweneizi CCM Ubungo Mbarouk Masoud akifanya utambulisho wa viongozi ngazi ya Wilaya na waliofuatana na Mgeni Rasmi.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Ndugu Mgonja.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo Masumbuko Maina akisalimia baada ya kutambulishwa
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ubungo Ndugu Mgonja akisalimia baada ya kutambulishwa
Katibu Msaidizi wa mkoa wa Dar es Salaam Stan Mkandawile akisalimia baada ya kutambulishwa
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mabibo Nasibu Mangushi akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa Bakwata Kata ya Mabibo Jafar Rajab akiongoza kuomba dua wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wakipokea Dua hiyo
Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Stan Mkandawile akijadili jambo na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Ubungo Ndugu Maina nje ya ukumbi wakati wa mkutano huo
Katibu wa UVCCM Kata ya Mabibo akisoma risala
Halafu ikaingia Burudani ya U-Miss👇
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Ndugu Mgonja akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba, akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo Wilayani Ubungo katika mkoa huo, Uliofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo Cha Usafirishaji (NIT), Mabibo, leo. Wajumbe wakimsikilia mgeni rasmi
Wajumbe na Waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi
Wajumbe na Waalikwa wakimsikilia mgeni rasmi
Wajumbe na Waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi
Mmoja wa waalikwa kwenye mkutano huo akipata chanjo ya Uviko 19 nje ya ukumbi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba akisindikizwa wakati akiondoka baada ya kufungua mkutano huo
"Haya nawatakia mkutano mwema", Mama Kate Kamba akiagana na viongozi
"Haya Mwenyekiti nenda salama", Mwenyekiti wa Ubungo Ndugu Mgonja akimuaga zaidi Mama kate Kamba
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Mama Kate Kamba akiwa tayari katika gari lake kwa ajili ya kuondoka kwenye mkutano huo.
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇