Na Bashir Nkoromo, Dodoma
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepitisha kwa kauli moja kwamba kilele cha Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM kitafanyika mkoani Mara Februari 5, 2022 na Mgeni Rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu shaka mwishoni mwa kikao cha NEC kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, imesema, Maadhimisho hayo yataanza Januari 23, 2022.
Kwa mujibu wa Shaka NEC imekubaliana kuwa uzinduzi rasmi utafanyika Januari 29, 2022, katika mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar na Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Mstaafu Dk. Ali Mohamed Shein.
Mbali na kupitisha hayo kwa kauli moja, NEC imempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia kwa kusimamia vema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020- 2025 kwa ustawi wa Wananchi wote wa Tanzania.
Aidha Taarifa hiyo imesema, NEC imewashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi kwa ujumla kwa kuendeleza Utulivu, Umoja na Mshikamano uliopo hapa nchini.
Your Ad Spot
Dec 18, 2021
Home
featured
siasa
KILELE CHA MIAKA 45 YA CCM KUFANYIKA MKOANI MARA, UZINDUZI KUFANYWA NA DK. SHEIN MKOA WA KUSINI UNGUJA JANUARI 29, 2022
KILELE CHA MIAKA 45 YA CCM KUFANYIKA MKOANI MARA, UZINDUZI KUFANYWA NA DK. SHEIN MKOA WA KUSINI UNGUJA JANUARI 29, 2022
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇