Michael Kadebe ameshinda kiti cha Urais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) baada ya kupata kura 58 na kumshinda Phares Magesa aliyekuwa anatetea nafasi yake ambaye alipata kura 8, kwenye uchaguzi uliofanyika jana Disemba 30, 2021 Jijini Dodoma.
Kwenye nafasi ya makamu wa Rais Rwehabura Barongo ambaye ni MVP wa kwanza wa michuano ya Sprite Bball Kings inayoandaliwa na East Africa TV na East Africa Radio, ameshinda nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura 44, akiwashinda Mboka Mwambusi aliyepata kura 9 na Alphonce Kusekwa kura 7.
Mwenze Fiston ameshinda nafasi ya katibu mkuu wa TBF kwa kura 47, akimshinda Michael Mwita 13 na nafasi ya katibu msaidizi ameshinda Benson Nyasebwa kwa kura 50 dhidi Daniel Kapomaaliyepata kura 10.
Wajumbe 60 ndio waliopiga kura kwenye uchaguzi huo, na safu mpya ya uongozi italiongoza shirikisho hilo kwa miaka 4 ijayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇