MSAJILI wa Baraza la Famasi Nchini,Elizabeth Shekalaghe ametoa onyo kwa Wamiliki wa Maduka ya Dawa za binadamu kuweka matangazo ya huduma katika milango ya maduka yao kwani ni kinyume na Sheria ya Baraza hilo huku akidai watakaobainika watafungiwa kutoa huduma.
Vilevile, ametoa wito kwa wanachi kuacha tabia ya kununua dawa kiholela kwani ni sumu na huleta madhara pale mtu anapotumia bila kufuata ushauri wa wataalamu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Desemba 10,2021,kuhusu matumizi holela ya dawa,Msajili huyo ametoa onyo kwa wamiliki hao kutoweka matangazo ya huduma katika milango ya maduka yao kwani ni kinyume na Sheria ya Baraza hilo.
“Kumekuwa na utaratibu watu kuweka mabango kwenye milango kana kwamba wanatoa matibabu au anaweka picha ya daktari kwamba tunatoa ushairi kana kwamba kuna huduma zinapatikana
“Niwaombe wamiliki wa maduka ya madawa kuacha mara moja na ndugu zangu nitakapopita na kukuta unatangaza, sheria tunapashwa kukufungia huduma,”amesema.
Aidha, amewataka Wafamasia ambao hawajahuisha leseni zao kufanya hivyo kabla ya Disemba 31 Mwaka huu kupitia mfumo wa kielektroniki.
“Sheria inawataka wanataaluma wote kufanya marejeo ya leseni zetu kwa mwaka sasa hivi tupo katika hatua nzuri kwani kati ya wafamasia 2597 ambao wamesajiliwa 2479 wamehuisha leseni zao sawa na aasilimia 93,”amesema.
Vilevile, ametoa wito kwa wanachi kuwa dawa ni sumuna huleta madhara pale mtu anapotumia bila kufuata ushauri wa wataalam wa afya hivyo waache tabia ya kununua dawa kiholela.
“Ni vema wananchi mkafahamu kuwa zipo athari za matumizi yasiyo sahihi ya dawa na athari zake ni kuongezeka kwa ugonjwa,kutokupata nafuu,kutokupona na hatimaye kupolekea kifo,”amesema.
Amewataka wananchi kuepuka kununua dawa kwenye maduka ambayo hayajasajiliwa na Baraza la Famasi kwani ubora wake ni wa mashaka na maelezo juu ya dawa hizo yanaweza kupotoshwa.
Pia amewataka wafamasia,mafundi sanifu wa dawa na wasimamizi kuzingatia sheria.
“Wafamasia wenzangu tuhakikishe tunasimamia misingi ya utoaji huduma kwenye taaluma hii ambayo tumeisomea,”amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇