Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene leo Novemba 26, 2021 amezungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu tulipotoka, tulipo na tunakoelekea na kuelezea changamoto na mafanikio kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofikia kilele Desemba 9,2021.
Simbachawene ameelezea mambo mbalimbali kuhusu mafanikio ya wizara hiyo, lakini pia amewatahadharisha polisi wasio waaminifu wanaowanyima watuhumiwa kutumia simu zao au za kituo cha polisi kuwajulisha ndugu zao kwamba wamekamatwa, amewataka kuacha mara moja tabia hiyo na atakayekiuka atachukuliwa hatua kali...
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza wakati Waziri Simbachawene akielezea mafanikio ya wizara hiyo.
Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha ITV Dodoma, Shaban Tolle akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.
Mwandishi wa habari wa Macho Media Online TV, Ahmad Said akiuliza swali kwa Waziri Simbachawene.
Ofisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Immaculate Makilika (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Simbachawene baada ya mkutano huo aliouongoza kumalizika.
Mwandishi wa habari wa Macho Media Online TV, Ahmad Said akiuliza swali kwa waziri wakati wa mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Simbachawene pamoja na mambo mengine akipiga marufuku polisi kuwanyima watuhumiwa kuwasiliana na ndugu zao kwa simu wawapo vituo vya polisi..
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇