LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 7, 2021

SIMBA YAMTANGAZA MHISPANIA PABLO FRANCO KUWA KOCHA WAKE MKUU MPYA

CCM Blog, Msimbazi

Klabu ya Simba ya Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam, imemtambulisha rasmi Raia wa Hispania Pablo Franco MartĂ­n kuwa kocha Mkuu wake kubeba mikoba ya Didier Gomes da Rosa aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni.

Franco mwenye umri wa miaka 41 ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi Real Madrid mwaka 2018, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Klab hiyo ya Simba.

Mhispania huyo huyo, kabla ya kujiunga na Klab hiyo ya Simba alikuwa Kocha wa Klab ya Al Qadsia ya Kuwait na amewahi kuwa pia kuwa Kocha wa Getafe mwaka 2015.

Hispania Pablo Franco MartĂ­n

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages