LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 23, 2021

SH MIL 60 ZA UVIKO 19 (IMF) ZASAIDIA KUTATUA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA, MUSOMA VIJIJINI+video

Kiriba Sekondari ni ya Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 - Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba.


Sekondari hii inajiandaa kupokea WANAFUNZI 431 wa Kidato cha kwanza mwakani (January 2022). Kwa hiyo, bila FEDHA za UVIKO 19 (IMF), baadhi ya Wanafunzi wa Sekondari hii wangelazimika kusomea chini ya miti! 

WANAVIJIJI wa Kata hii wamehamasika na kuamua kuchangia NGUVUKAZI zao ili kazi ikamilike kwa wakati na FEDHA hizo (TSH MILIONI 60) ikiwezekana zivushe malengo yake.

WANAVIJIJI hao hao na WADAU wao wa MAENDELEO tayari wamekamilisha ujenzi wa MAABARA 3 nzuri za Fizikia, Kemia na Biolojia. 



TAARIFA nyingine itawafikia kuhusu uamuzi wa KATA ya KIRIBA kuomba Serikali ikubali kuanzisha "HIGH SCHOOL" ya Masomo ya Sayansi mwakani (Julai 2022) baada ya kukamilisha kujenga MIUNDOMBINU inayohitajika.

Karibu uchangie Maendeleo ya uhakika ya Jimbo la Musoma Vijijini. 

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz


Tafadhali wasikilize WANAVIJIJI na VIONGOZI wao na wa shule kwenye "CLIP" iliyoambatanishwa hapa.




 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages