LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2021

MBUNGE JANETH MAHAWANGA ATOA SOMO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI

Na Christopher Lisa-UMG

Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga, amevishauri vikundi vya wajasiriamali  kuwekeza katika kupata elimu zaidi na teknolojia  ili  kupata tija.

Ushauri huo ameutoa, katika Jimbo la Ukonga wakati akifungua kongamano la Vijana na Ujasiriamali  liloandaliwa na Taasisi ya  Tuamke Pamoja Tanzania, katika Jimbo la Ukonga.

Mbunge Janeth amesema, suala la mitaji si changamoto tena  kwa  wajasiriamali kwani serikali inatoa mikopo  isiyo na riba  kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu  wenye ulemavu kupitia gawio la asilimia 10 linalotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kote nchini.

“Kikubwa  wajasiriamali wekezeni katika kujifunza. Mshirikini katika mafunzo ili mtambue fursa,”amesema Mbunge huyo.

Amebainisha, pia  wajasiriamali wawekeze katika Teknolojia  ambayo ndiyo msingi mkubwa katika kufikia tija kwa sasa.

“Kijana mjasiriamali unamiliki simu janja.  Jiulize unaitumiaje simu hiyo katika kukuletea fursa? Pia ni lazima uwe na juhudi maarifa na uthubu,”ameeleza Mahawanga.

Ameeleza  katika suala la uwezeshaji , vijana wanawake na watu wenye ulemavu mkoani  Dar es Salaam, anamatarajio makubwa ya kuona matokeo chanya ili  kuendana na kasi ya  Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo.

Amewataka wajasiriamili popote walipo kuwasiliana naye ili kusaidiana katika kufanikisha uundwaji wa vikundi, usajili wa  hata kunapokuwa na mkwamo wa kupata mikopo.

“Kazi yangu mimi siyo kwenda t u Dodoma. Kazi yangu ni kuwatumikieni nyinyi wananchi. Niiteni mtaani kwenu.  Siyo lazima katika ukumbi hata kwenye mikeka tutakaa. Tujadili masuala ya ujasiriamali. Nataka kuona Dar es Salaam, ikifanikiwa katika hili,”amebainisha.

Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya  Tuamke Pamoja Tanzania, Nasra Msofe, alisema taasisi hiyo inahudumia vikundi nane vya ujasiriamali na imejikita kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana pamoja na kujitambua.

“Tunataka kuendana na sera ya serikali yetu chini ya Rais Samia ya Uchumi wa Viwanda, hivyo tumejikita katika kuhamasisha jamii    kufanya ujasiriamali na kutafuta masoko ya biashara ,”ameeleza

Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga, akizungumza  wakati akifungua Kongamano la Vijana na Fursa lililokuwa limeandaliwa na Taasisi ya  Tuamke Pamoja Tanzania, katika Jimbo la Ukonga.

Picha: Mbunge Janeth Mahawanga akiwa katika matukio mbalimbali wakati akizindua Kongamano hilo 👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages