LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2021

DAR MABINGWA WA CRDB BANK BASKET TAIFA CUP 2021+video

Mabingwa wa mashindano ya Taifa ya mpira wa kikapu ya CRDB BANK BASKET TAIFA CUP wakishangilia baada kukabidhiwa kombe na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi wakati wa kilele cha mashindano hayo kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma Novemba 14, 2021.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano hayo, Nahodha wa timu ya Mkoa wa Dar es Salaam wanaume, Omary Mohammed.

Mabingwa wakifurahia baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 6.5 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano hayo, Nahodha wa timu ya Mkoa wa Dar es Salaam wanawake, Khadija Karambo
Nahodha Khadija Karambo akilinyanyua kwa furaha Kombe la ubingwa mara baada ya kukabidhiwa.

Timu ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa na hundi ya sh. mil.6.5 baada ya kukabidhiwa na wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Benki ya CRDB.

Naibu Waziri, Ndejembi akiwavisha medali wachezaji wa timu ya Arusha wanaume baada ya kuwa washindi wa pili katika mashindano hayo. Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mboka Mwambusi.
Ndejembi akimkabidhi tuzo maalumu Mkurugenzi wa Masoko wa PSSSF,  James Mlowe kwa kutambua mchango wa udhamini wa mashindano hayo.
Ndejembi akimvisha medali mwamuzi wa kimataifa wa mchezo wa mpira wa kikapu, Daliso Mwidadi.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



TIMU za mpira wa kikapu za wanawake na wanaume Mkoa wa Dar es Salaam zimetwaa ubingwa wa mashindano ya Taifa ya CRDB Bank Basket Taifa Cup yaliyofikia kilele kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma Novemba 14,2021. Katika kilele cha mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Benki ya CRDB, mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi. Ndejembi aliwakabidhi vikombe vya ubingwa wa mashindano hayo, Nahodha wa timu ya Dar wanaume, Omary Mohammed na Khadija Karambo wa timu ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na kuwapatia kila moja zawadi ya sh. milioni 6.5. Pia wachezaji bora na waamuzi bora wa mashindano hayo walikabidhiwa tuzo na zawadi ya fedha taslimu. Timu zlitoingia fainali kwa upande wa wanaume ni Dar es Salaam na Arusha na kwa upande wa wanawake ni Dar es Salaam na Unguja.


Mdau, nakuomba uendelee kushuhudia fainali za mtanange huo, Dar wanawake dhidi ya Unguja na Dar wanaume dhidi ya Arusha....
 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages