LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 4, 2021

CRB YATAKA MAKANDARASI KUJAZA TENDA KIELEKTRONIKI TANePS

Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akiwasili kwaajili ya kufungua mkutano wa makandarasi wazalendo mkoani Iringa jana kuhusu ujuzi wa biashara. Kushoto ni Meneja wa CRB, Kanda ya Kusini Mhandisi Ally Mwita na Mratibu wa mafunzo CRB Neema Fuime. Kulia ni Naibu Msajili CRB, David Jere
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akifungua mkutano wa makandarasi wazalendo mkoani Iringa jana kuhusu ujuzi wa biashara. Kushoto ni Meneja wa CRB, Kanda ya Kusini Mhandisi Ally Mwita na Mratibu wa mafunzo CRB Neema Fuime. Kulia ni Naibu Msajili CRB, David Jere
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akiwa kwenye picha ya pamoja na makandarasi wazalendo mara baada ya kufungua mkutano wa siku tatu kwa makandarasi wazalendo mkoani iringa
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akizungumza na Mratibu wa Mafunzo wa bodi ya makandarasi (CRB), Neema Fuime kushoto na kulia Msajili Msaidizi wa CRB, David Jere baada ya kufungua mafunzo kwa makanadarasi wazalendo mkoani iringa

  Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa akifungua mafunzo hayo ya siku tatu mkoani Iringa


Na Mwandishi Wetu, Iringa

MAKANDARASI nchini wametakiwa kuufahamu na kuutumia mfumo wa serikali wa kuomba zabuni kielektroniki (TANePS) kwani zabuni zote zimekuwa zikiombwa kupitia mfumo huo.

Hayo yalisemwa jana mjini Iringa na Mwenyekiti wa Bodi  ya Makandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wazalendo wa  nyanda za juu kusini mkoani Iringa kuhusu usimamizi wa biashara.

Alisema kwa kuwa mtoaji wa zabuni nyingi ni serikali hakuna namna ambayo makandarasi hao wanaweza kukwepa kuujua mfumo huo kwani zabuni zote za serikali zinaombwa kupitia mfumo huo wa kielektroniki.

Kadhalika, aliwataka kuisoma mikataba kwa umakini mkubwa kabla ya kuisaini ili kuepuka kuingia kwenye mikataba ambayo wanaweza kushindwa kuitekeleza na kukimbia miradi wakati wa kuitekeleza.

Mhandisi Ngimbwa alisema ni vyema mkandarasi akajiridhisha na mkataba anaoingia kwa kuusoma vizuri na kama haelewi kuomba ufafanuzi ili asijiingize kwenye mkataba ambao hataweza kuutekeleza.

Alisema baadhi ya makandarasi wamekuwa wakiwapa watu hasa wahandisi kuwajazia zabuni hali ambayo imesababisha wakose zabuni hizo kutokana na kujazwa bila kufuata taratibu.

“Msiwape watu wengine wawajazie na mkipata zabuni msome mikataba kwa umakini msikimbilie kusaini tu mwishowe mnalalamika kumbe yale mliyolalamikia yalikuwepo wakati unasaini,” alisema

“Unakuta kwenye zanuni umeambiwa ueleze uzoefu wa miaka mitano wewe unajaza uzoefu wa miaka mitatu halafu unasubiri upate zabuni na ukikosa unalalamika wakati hukukidhi vigezo,” alisema Mhandisi Ngimbwa

Aliwataka makandarasi kuungana ili waweze kuwa na nguvu ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi kwani hata makampuni makubwa ya wachina yamekuwa yakiungana kwaajili ya kutekeleza miradi mikubwa.

Alisema makandarasi wengi wamekuwa wakiogopa kuingia kwenye kufanya kazi kwa ubia kwa kuhofia kupata hasara lakini alisisitiza kuwa ubia haukwepeki kwani ndiyo jawabu la mafanikio ya makandarasi wazalendo.

“Kazi za ubia zinachanagamoto zake lakini msiogope kufanyakazi kwa umoja kwasababu ukiwa kwenye ubia kuna mambo mengi unajifunza na unapata uzoefu wa kutosha kufanya miradi mikubwa,” alisema

Aliwataka pia kuachana na utaratibu wa kuwa na vyama vingi vya makandarasi na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu ambacho kitakuwa sauti yao wanapokuwa na matatizo na changamoto mbalimbali kwa serikali au kwa wateja wao.

Meneja wa CRB nyanda za juu kusini, Mhandisi Ally Mwita alisema wateja wanapaswa kuwalipa makandarasi kwa wakati ili waweze kutekeleza miradi wanayopewa kwa wakati uliopangwa na kwa ufanisi.

“Umempa mkandarasi zabuni ametumia fedha zake na amekamilisha unapaswa kumlipa kwa wakati ili nayeye alipe wanaomdai na kushindwa kufanya hivyo ni kumdhoofisha mkandarasi” alisema

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages