Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Dkt Tim Kelly kutoka Marekani ambaye yupo nchini na jopo lake kutathmini maandalizi ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano nchini. Benki ya Dunia imetoa mkopo wa masharti nafuu sh. bilioni 349 za kugharamia uboreshaji wa miundombinu hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama, Samson Mwera akizungumza wakati wa mkutano huo kuhusu mikakati iliyowekwa kutekeleza kwa ufanisi uboreshaji huo kufikia Tanzania ya Kidijitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Benadickt Ndomba akielezea jinsi walivyojiandaa kwa ajili ya uboreshaji wa mitandao nchini kwa kutumia fedha hizo.
Naibu Waziri, Kundo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Dkt Tim Kelly wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu wa wizara na maofisa wa Benki ya Dunia.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Prisca Ulomi akiwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Dkt Tim Kelly.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue kilichozungumzwa na Naibu Waziri Kundo, viongozi wa taasisi na ofisa wa Benki ya Dunia.....
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇