LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2021

WIZARA, MA RAS WAJIPANGA KUONGEZA KASI UWEKAJI ANUANI ZA MAKAZI+video

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab Chaula akizungumza  wakati wa mkutano na Makatibu Tawala wa Mikoa 26 Tanzania Bara jijini Dodoma leo Oktoba 21, 2021, kuhusu uwekaji wa mpango mkakati wa pamoja wa kuongeza kasi ya uwekaji wa anuani za makazi nchini, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo akielezea jinsi wizara hiyo ilivyojipanga kuhusu mpango huo wa uwekaji wa anuani za makazi nchini.
Kamishna wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Mathew Nhonge akielezeaa jinsi walivyojipanga
Mratibu wa Kupanga, kupima na kumilikisha ardhi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godfrey Machabe akielezea vigezo vilivyotumika kuteua halmashauri 55 itakazopatiwa fedha za mkopo kwa ajili ya kupanga na kupima pamoja na kumilikisha ardhi na miji ili kurahisisha mpango wa uwekaji  anuani za makazi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akichangia mada kwa kutoa ushauri mpango wa anuani za makazi kuufanikisha haraka kwa kiasi kidogo cha fedha kilichopo. 


Mkurugenzi wa Mawasiliano wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akisoma  maazimio 10 ya mkutano huo yenye lengo la kuongeza kasi  ya kuweka anuani za makazi nchini.
Makatibu Tawala wa  mikoa wakiwa katika mkutano huo.







Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Dkt Angelina Lotambi  akitoa ushauri wake kuwa fedha kidogo zilizotengwa kwa ajili ya mpango wa anuani za makazi zigawiwe sawa katika mikoa yote nchini ili kazi ienze mara moja.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Dkt Athuman Kihamia  akishauri katika mgawo wa fedha hizo hata majiji yapewe.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa  Faustine Kamuzora akielezea jinsi mkoa huo ulivyofanikiwa kuweka anuani za makazi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngussa Samike (kushoto  akielezea jinsi mkoa huo ulivyofanikiwa kuweka anuani  za makazi pamoja na kuishauri serikali inapotuma fedha za maendeleo katika halmashauri, taarifa pia ipelekwe  kwa makatibu tawala wa mikoa.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini ujue yaliyojiri na maazimio ya mkutano huo.....
 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages