Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki na wanachama wawekezaji wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama(hayupo pichani) wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda,akieleza jambo wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya JATU PLC Peter Gasaya,akielezea mikakati wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya JATU PLC, Dkt. Zaipuna Yonah,akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda,akiipongeza Kampuni ya JATU wakati wa hafla hiyo ya ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia) akizindua rasmi mradi wa Ufugaji, Bima na Bank ya kampuni ya JATU PLC. Wa tatu kutoka kushoto ni Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya JATU PLC, Dkt. Zaipuna Yonah ikiashiria mchango wake mkubwa katika malenzi ya vijana wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi tuzo Msanii wa Muziki na Balozi wa kampeni ya ANZA NA EKARI MOJA inayoratibiwa na JATU PLC baada ya kuibuka kidedea katika uhamasishaji wa shughuli za kampuni hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na Wadau wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka Mitano (5) ya Kampuni ya JATU PLC iliyofanyika tarehe 23 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia ni Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda (kulia). Kushoto aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya JATU PLC, Bw. Peter Gasaya na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya JATU PLC, Dkt. Zaipuna Yonah.
………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza kufurahishwa na kasi ya uwekezaji wa wanachama katika kampuni ya JATU PLC na namna inavyowakomboa vijana kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Pongezi hizo zilitolewa jana Oktoba 23, 2021 jijini Dodoma na Waziri Mhagama wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 5 ya kampuni hiyo toka ianzishwe mwaka 2016.
Waziri Mhagama amefafanua kuwa, Kampuni ya JATU PLC imekuwa kiuongo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi kupitia miundombinu thabiti iliyojiwekea ambayo imejikita katika shughuli za kilimo, viwanda na masoko hivyo zimekuwa ni msaada mkubwa kwa wanachama kuondokana na umaskini.
“JATU PLC ni kampuni iliyoanzishwa na vijana, nafurahi kuona mmeweza kushiriki katika juhudi hizi za Serikali kwa kuhakikisha mnazalisha malighafi na kuongeza thamani ya Mazao mnayozalisha kupitia Viwanda kwa lengo la kuwa na mnyororo wa kuongeza thamani na kulinda ajira za vijana wetu ili kupitia mnyororo huo wa thamani muweze kutoa ajira nyingi na kujipatia kipato,” amesema Waziri Mhagama
“Nipongeze kampuni ya JATU PLC kwa namna imekuwa ikiwasaidia vijana kuondokana na changamoto mbzlimbali zinazowakabili kwa kuwashirikisha katika kilimo, ufugaji na miradi mbalimbali inayoratibiwa na kampuni hiyo maana imewawezesha vijana kuleta mageuzi ya maendeleo katika Taifa lao,” amesisitiza Waziri Mhagama
Aidha amesema kuwa utafiti wa nguvukazi uliofanyika 2014 ulibainisha asilimia 56 ni vijana hivyo kupitia fursa ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na kampuni ya JATU PLC ni vyema ikatumika kuwasaidia vijana kuondokana na changamoto ya ajira kwa kuwashiriki katika miradi ambayo itawaletea matokea yenye tija.
“Serikali itaendela kuhakikisha kuwa inawawekea vijana mazingira mazuri kupitia program zake mbalimbali ambazo zitawawezesha kupata elimu, ujuzi na mitaji ambayo itawasaidia kujiajiri na kuajiri wenzao,” amesema
“Serikali pia itaendelea kuwasadia vijana wa JATU ili kuhakikisha wanafikia malengo yao,”
Hata hivyo amesema kuwa, Malengo ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Vijana yameainishwa katika nyaraka na miongozo mbalimbali ikiwemo Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2020 -2025, Dira ya maendeleo ya Taifa (vision 2025), Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 2030; Agenda ya Umoja wa Nchi za Afrika 2063; Sera ya Maendeleo ya Viwanda; Sera ya Taifa ya Ajira ya Mwaka 2008
Pia ametoa rai kwa vijana wote nchini wahitimu wa vyuo vikuu, vyuo vya kati, Sekondari na hata msingi kujiunga katika vikundi na kusajili Kampuni au vikundi vyao ili waweze kusaidiwa kwa urahisi na waweze kutimiza ndoto zao.
“Vijana mnapaswa kuiga kazi nzuri zinazofanywa na vijana wenzenu waliopo JATU PLC. Ili kuliwezesha taifa letu kufikia azma yake ya kufikia uchumi wa kati wa juu,” alisema Mhagama
Katika hatua nyingine Waziri Mhagama amewapongeza wakezaji katika kampuni hiyo na aliwasihi kuendelea kuongeza mtaji na kupanua wigo wa biashara zao.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda amesema kuwa kutokana na ukubwa wa kampuni ya JATU PLC ni mafanikio iliyonayo vi vyema vijana wakachangamikia fursa hiyo ili wajikwamue kiuchumi.
“Katika hafla hii tumejifunza mengi kwa kuona kampuni ya JATU PLC inavyotekeleza mikakati yake kwa ufasaha hivyo Vijana mkawekeze JATU,” amesema Mhe.Pinda
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamisi Munkunda ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kwa namna ofisi yake imekuwa mlezi mzuri kwa kampuni hiyo ya JATU PLC ambayo imepelekea mafanikio hayo yaliyofikiwa katika miaka mitano.
“Katika miaka mitano JATU PLC inajivunia mafanikio iliyoyapata ambayo yamewezesha kampuni kufungua rasmi mradi wa Ufugaji, Bima na Bank ambayo itatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kutekeleza miradi yao kwa ufanisi na usalama,” amesema Gasaya
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇