LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 8, 2021

WAZIRI DKT KIJAJI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA POSTA AFRIKA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Sifundo Moyo ambaye alimtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt Zainab Chaula.

Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Posta Afrika, Dkt Moyo amempatia taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Posta Afrika  jijini Arusha litakalokuwa la ghorofa 17,  kuwa hadi sasa ujenzi wake umefikia ghorofa 12.

Dkt. Moyo  atahudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani kesho Oktoba 9, ambayo kwa hapa nchini yatafanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango. 


Waziri Kijaji (katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na Katibu Mkuu wa PAPU, Sifundo Moyo Katibu Mkuu wa  wizara hiyo, Dkt Chaula na maafisa wa PAPU na wizara hiyo.
Waziri Kijaji akizungumza na mgeni wake, Katibu Mkuu wa PAPU, Moyo.
Waziri Kijaji akiongoza mazungumzo na maafisa wa PAPU na wa wizara hiyo ofisini kwake Mtumba.




 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages