LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 5, 2021

WALIMU WATAKIWA KUVUTA SUBIRA AHADI YA RAIS SAMIA KUPANDISHA MISHAHARA+video

 KAIMU Rais wa Chama Cha Walimu (CWT) Dinnah Mathaman amewaasa  walimu kuwa subira kutokana na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuongeza  mishahara ya watumishi  aliyoitoa mwaka huu kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei Mosi) iliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza.


Mathaman aliyasema hayo jana jijini hapa katika maadhimisho ya siku ya walimu yaliyoandaliwa na CWT Mkoa wa Dodoma .

Alisema ,licha ya changamoto ya walimu iliyopo nchini lakini bado wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuipa serikali hamasa ya kuongeza mishahara hiyo.

Aidha alisema moja ya changamoto inayowakumba walimu Duniani ni changamoto ya upungufu wa walimu ambapo kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Maendeleo ya Duniani kuna upungufu wa Walimu milioni 69 Duniani.

Alisema,walimu wana kila sababu ya kuchapa kazi kutokana na Serikali kuwajali katika masuala yao ya kila siku ikiwemo upndishwaji wa madaraja,ulipaji wa madeni hivyo wanapswa ahadi ya uongezwaji mishahara iliyotolewa na Rais .

Mathaman alisema,lengo lao ni kuona walimu wanafanyia kazi kwa bidii ili kuisaidia serikali kuinua kiwango cha Elimu hapa nchini.

Hata hivyo aliwataka walimu kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili kuhakikisha zinakwish na wazo kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni,yartibu na sheria zilizopo.

Akizungumza kuhusiana na upungufu wa Walimu Mathaman alisema ,hilo ni tatizo la kidunia na kwamba changamoto hiyo isiwatie hofu badala yake waitumie kama fursa kuhakikisha wanafanyia kazi kwa bidii.

Naye Jaji Mathew Mwalimu kutoka Sekretarieti  ya Maadili alisema walimu ni chombo muhimu na hakuna kiongozi yeyote ambaye hajapita kwenye mikono ya mwalimu hivyo walimu wana kila sababu ya kukuona wao ni mstari wa mbele katika kuinua Taifa.

Alisema,hata yeye taaluma yake ni mwalimu kabla ya kuwa Maji hivyo uwepo wake katika maadhimisho hayo ni kama sekretarieti ya maadili inayojihusisha na kutoaatamko mbalimbali.

Kutokana na hilo aliwapongeza walimu kwa kuadhimosh siku yao huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha sekta ya ualimu inasonga mbele.

"Walimu msijione wanyonge,na badala yake mnapaswa kutembea kifua mbele maana watu wote wakiwemo viongozi wakubwa wamepita kwenye mikono yenu na kuwepo hapo waliopo." Alisema Jaji Mathew.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Kaimu Rais wa CWT Mathaman  akizungumzia suala hilo....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages