Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga (kulia), Mkulima Steven Marealle pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA), Dkt Sophia Kashenge alipokuwa akikabidhi tani 1600 za mbegu za alizeti zilizoandaliwa na Wakala wa Mbegu nchini (ASA) katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma Oktoba 23,2021.
Wayiri Mkenda ametangaza punguzo kubwa la mbegu hizo kwamba badala kuuza kwa bei ya sh 35,000 kwa kilo sasa itauzwa kwa wakulima wa zao hilo sh. 3,500 kupitia halmashauri za mikoa ya Dodoma, Singida, Simiyu, Manyara na Kilimanjaro.
Mara baada ya kutangaya bei hiyo ziliibuka shangwe na vigelegele kutoka kwa baadhi ya wakulima waliohudhuria makabadhiano hayo.
Waziri Mkenda na viongozi wengine wakiwa pamoja na baadhi ya wakulima wenye furaha ya kukabidhiwa mbegu ya alizeti.
Baadhi ya wakulima wakiwa katika hafla hiyo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akielezea mkakati wa mkoa huo ulivyojipanga katika kilimo cha alizeti.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel akiishukuru Serikali kuwapatia mbegu ya alizeti kwa bei poa.
Waziri Mkenda akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu ya alizeti kwa wakulima.
Mkulima mkubwa wa alizeti, Steven Marealle akitoa shukrani kwa serikali kuwakumbuka wakulima kwa kuwapatia mbegu ya alizeti kwa bei poa.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini, Waziri Mkenda, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda wakizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hizo ......
Imeandaliwa na Richard MwaikendaMhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇