LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2021

VIPAJI FOUNTAIN GATE ACADEMY VYAMSHANGAZA AFISA ELIMU ILALA

 Mwanafunzi bora wa jumla katika taaluma wa shule ya Fountain Gate Academy ya Tabata, Mulan Matatizo akipokea cheti kutoka kwa Afisa Elimu Manispaa ya Ilala anayehusika na jusajili wa shule, Asha Mapunda wakati wa mahafali ya tisa yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi

     Wahitimu wa shule ya awali Fountain Gate Academy wakionyesha vipaji vyao wakati wa mahafali ya tisa yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Elimu Manispaa ya Ilala anayehusika na jusajili wa shule, Asha Mapunda

 Kikundi cha House of Talent cha shule ya Fountain Gate Academy kikionyesha manjonjo yake wakati wa mahafali ya tisa shuleni hapo siku ya Jumamosi ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Elimu Manispaa ya Ilala anayehusika na jusajili wa shule, Asha Mapunda

 Kikundi cha karate cha cha shule ya Fountain Gate Academy kikionyesha manjonjo yake wakati wa mahafali ya tisa shuleni hapo siku ya Jumamosi ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Elimu Manispaa ya Ilala anayehusika na jusajili wa shule, Asha Mapunda




   


   

Vipaji Fountain Gate Academy vyamshangaza Afisa Elimu Ilala

Na Mwandishi Wetu

AFISA Elimu Wilaya ya Ilala, Asha Mapunda ameelezea kushangazwa kwake na vipaji vya wanafunzi wa shule ya msingi na awali ya Fountain Gate Academy ya Tabata  huku akiipongeza kwa kuubeba Mkoa wa Dar es Salaam kwenye matokeo ya kitaifa.

Asha anayeshughulikia usajili wa shule za binafsi na za serikali Wilaya ya Ilala aliyasema hayo siku ya Jumamosi wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi ya fountain Gate.

Alisema wanafunzi wadogo lakini wameonyesha umahiri mkubwa kwenye kuelezea mambo ya kisayansi kiasi cha kumshangaza kwa kiwango kikubwa.

Alisema ni mara yake ya saba kufika shuleni hapo kwenye mahafali ya shule ya msingi na awali lakini uwezo walionyesha mwaka huu kwenye maonyesho ya kitaaluma ni mambo makubwa sana ambayo mtu mwingine anaweza asiamini

“Hii ni mara yangu ya saba kuja hapa lakini haya yaliyofanyika leo ni fungakazi, maana mwanafunzi wa shule ya awali anazungumza mambo makubwa ya kitaaluma tena kwa lugha ya kiingereza fasaha utadhani ni wa sekondari nawapongeza sana,” alisema

Aidha, alisema umahiri wa wanafunzi hao unadhihirisha ubora wa walimu wa shule hiyo huku akiwataka walimu kutobweteka na badala yake waendeleze mambo mazuri yanayofanyika.

Alisema shule hiyo imekuwa ikiusaidia sana Mkoa wa Dar es Salaam kufanya vizuri kitaifa kila yanapotoka matokeo ya mitihan I ya kitaifa hivyo inajivunia uwepo wake kwenye Wilaya ya Ilala.

“Ukisikia Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa kwanza basi Fountain Gate imekuwa msaada mkubwa sana kwasababu imekuwa ikiwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na nawaomba mchukue nafasi ya kwanza maana hiyo ni yenu,” alisema

Mkurugenzi wa shule hiyo, Japhet Makau alisema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma na aliwaahidi wazazi kwamba hawatabweteka na wataendelea kufanya vizuri.

Alisema mbali na ubora wa taaluma shuleni hapo shule hiyo imekuwa ikiibua vipaji vya wanafunzi kwenye Nyanja mbalimbali kama sanaa, michezo na utamaduni .

Alisema kwa kuibua vipaji mbalimbali wamefanikiwa kuwa na timu ya mpira wa miguu inayocheza ligi daraja la kwanza na timu ya mpira wa miguu ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages